LIVE STREAM ADS

Header Ads

Mwanza watakiwa kuandaa eneo maalum la Maonesho ya Biashara Afrika Mashariki

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Online Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Adam Malima amewaagiza wakuu wa wilaya za Ilemela na Nyamagana kutafuata maeneo rasmi kwa ajili ya kufanyia Maonesho ya Biashara ya Afrika Mashariki.

Malima aliyasema hayo Agositi 29, 2022 wakati akifungua Maonesho ya 17 ya Biashara Afrika Mashariki yanayoandaliwa na chemba ya biashara, kilimo na viwanda Tanzania (TCCIA) yanayofanyika katika uwanja wa Nyamagana, kuanzia Agosti 26 hadi Septemba 04, 2022.

"Hatuwezi kuendelea kufanya maonesho kwenye uwanja wa mpira hivyo suala la kuwa na maeneo rasm ni la muhimu na itachochea zaidi wafanyabiashara kutoka nchi mbalimbali kuja kuonesha bidhaa zao" alisema Malima.

Malima alieza kuwa Mwanza ni mji wa kibiashara, viwanda na utalii hivyo maonyesho hayo yanatakiwa kuwa ya kihistoria katika kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.

Kwa upande wake Makamu wa Rais TCCIA, Clement Chiboko alisema kukiwa na eneo maalum kwa ajili ya maonesho hayo itasaidia kuongeza tija kwa wafanyabishara kuwekeza miundombinu bora zaidi kwa ajili ya bidhaa zao.

Naye Mwenyekiti wa TCCIA Mkoa Mwanza, Gabriel Chacha alisema pamoja na maonesho hayo kuwa na mafanikio makubwa kwa kuwaunganisha wafanyabishara na kukuza masoko yao katika nchi za Afrika Mashariki, bado yanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo wafanyabiashara kutoka nje ya nchi kucheleweshwa mpakani wanapokuwa na bidhaa wanazoleta kwenye maonesho.

Florah Magabe ambaye ni mwaandaaji wa kipindi cha 'Konzi la Moyo TV Show' kinacholenga kutoa elimu ya ukatili wa kijinsia alitumia fursa hiyo ya maonesho kuto wito kwa wahanga wote wa ukatili kufika kwenye maonesho hayo na kutembelea banda la taasisi yake ili wapate elimu na ushauri juu ya kukabiliana na vitendo vya ukatili wa kijinsia.

Washiriki wa maonesho Maonesho ya Biashara Afrika Mashariki wanaamini hiyo ni fursa nzuri ya kuwakutanisha pamoja kutangaza bidhaa zao huku wakipanua zaidi mtandao wao kimasoko na hivyo kuishukuru TCCIA kwa kuandaa Maonesho hayo mwaka wa 17 sasa.
Mwenyekiti wa TCCIA Mkoa wa Mwanza, Gabriel Chacha akizungumza kwenye Maonesho ya Biashara ya Afrika Mashariki.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Adam Malima (katikati) akikagua bidhaa za viatu katika banda la 'Konzi la Moyo TV Show'. 
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Adam Malima (wa pili kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi mbalimbali akiwemo Mwenyekiti wa TCCIA (kulia), Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Amina Makilagi (wa tatu kulia), Mwenyekiti UWT Mkoa Mwanza Hellen Bogohe (kushoto) pamoja na mwandaaji wa kipindi cha 'Konzi la Moyo TV Show', Frolah Magabe (kushoto nyuma).
Mwandaaji wa kipindi cha 'Konzi la Moyo TV Show', Florah Magabe.
Na Hellen Mtereko, Mwanza

No comments:

Powered by Blogger.