LIVE STREAM ADS

Header Ads

Wizara ya Madini kuhamasisha watanzania kushiriki michezo

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Online Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Serikali kupitia Wizara ya Madini inatarajia kuanzisha mashindano ya mchezo wa mbio utakaojulikana kama ‘Tanzania Madini Marathon’ ifikapo Mwaka 2023 ili kuhamasisha watanzania kushiriki katika michezo maeneo mbalimbali nchini.
Hayo yalibainishwa na Waziri wa Madini, Dkt. Doto Biteko baada ya kushiriki kwenye mbio za Shinyanga Madini Marathon ziliyofanyika Agosti 14, 2022 mkoani Shinyanga.

Dkt. Biteko alisema mwaka 2023, Serikali itaifanya Tanzania Madini Marathon kuwa ya kitaifa kwa kuwakutanisha wadau wa Sekta ya Madini na Sekta nyingine ili kushiriki kwa pamoja.

Alitumia fursa hiyo kumpongeza Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Sophia Mjema kwa kuandaa vizuri Shinyanga Madini Marathon ambayo imekuwa ya kwanza hapa nchini kuanzishwa.
Pia Dkt. Biteko alitoa tuzo, medali na zawadi kwa washindi mbalimbali wa mbio fupi na ndefu, mbio za kukimbia na beisikeli pamoja na mashindano mengine ambao wamefanya vizuri na kumaliza mashindano.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mjema aliipongeza Wizara ya Madini kwa kushirikiana pamoja katika shughuli hiyo katika mkoa huo. Amesema kupitia marathon hiyo imeweza kuweka ukaribu wa Serikali na wananchi katika kufanya mazoezi ili kujenga mwili.

Mbio za Shinyanga Madini Marathon 2022 zimekuwa za kwanza kuanzishwa hapa nchini katika Mkoa wa Shinyanga na kushirikisha riadha km 21, km 10, km 5 na km 2.5 pamoja na mbio za beisikeli.
Na Steven Nyamiti, WM

No comments:

Powered by Blogger.