LIVE STREAM ADS

Header Ads

Chama cha Wauguzi Tanzania chapata uongozi mpya

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Online Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Chama cha Wauguzi Tanzania (TANNA) kimefanya uchaguzi na kuwapata viongozi wake wakuu huku wakiomba Wizara ya Afya kuwezesha kada hiyo kutambulika nchini kutokana na umuhimu wake mkubwa kwa jamii.

Katika uchaguzi huo uliofanyika jijini Dodoma, Alexander Baluhya alichaguliwa kuwa Rais, Jane Bararukiririza kuwa Mamu wa Rais, Katibu ni Samwel Mwangoka na Katibu Msaidizi ni Steven Brown.

Vilevile Emilia Mwakanyanga akachaguliwa kuwa Mhazini na Msaidizi wake ni Yohana Bayo huku Meshack Makojijo akichaguliwa kuw Katibu Mwenezi na Msaidizi wake ni Prosper Kamazima.

Baluhya alisema kutotambuliwa kwa kada hiyo katika ngazi za Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) imekuwa ikiwavunja moyo kwa kiasi kikubwa.

Katibu Mkuu Wizara ya Afya Prof. Abel Makubi alisema changamoto zote zinazowakabili wauguzi zitatatuliwa na hivyo kuwataka kufanya kazi kwa bidii ili kuwezesha watanzania kupata huduma sitahiki za afya.

Alisema kwa sasa magonjwa ya kuambukiza na yasiyoambukiza yameongezeka nchini na hivyo kuwataka wauguzi kusaidia kuhamasisha wananchi kujiunga na mifuko wa bima ya afya ili kupata huduma bila adha.
Na Neema Kandoro, Dodoma

No comments:

Powered by Blogger.