SACCOS, AMCOS kuwezesha kidijitali Mwanza
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Online Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Kuwepo kwa mifumo inayowezesha vyama vya ushirika kufanya kazi zake vizuri kutaleta mabadiliko chanya ya maendeleo ya taasisi hizo zinazotegemewa na wananchi wengi katika shughuli zao za kila siku hapa nchini.
Hayo yalibainishwa Oktoba 19, 2022 na Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya Tanzania Mentors Actors (TMA), Paul Michael wakati wa kusaini makubaliano na taasisi ya Chipua Associates ya jiji la Mwanza kwa ajili ya kushirikiana kuvijengea uwezo wa vyama vya ushirika mkoani Mwanza.
Alisema TMA kwa kushirikiana na Serikali imewekeza katika mfumo wa kiteknolojia uitwao 'Speedy Finances' ili kutatua changamoto za usimamizi na utoaji huduma za kifedha kwenye SACCOS, AMCOS na taasisi mbalimbali za kifedha nchini.
Alibainisha kuwa, taasisi yake ya TMA kuungana na ile ya Chipua Associates kutaongeza ufanisi mkubwa wa kuzihudumia taasisi hizo ambazo ni mhimili kwa maendeleo ya wananchi.
Na Neema Kandoro, Mwanza
No comments: