LIVE STREAM ADS

Header Ads

Serikali kukamilisha zaidi ya miradi 1,000 ya maji

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Online Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga amesema Serikali inajenga zaidi ya miradi 1,000 katika maeneo mbalimbali kote nchini ili kuwasogezea huduma ya majisafi na salama wananchi.

Mhandisi Sanga alisema hayo Oktoba 13,2022 wakati wa hafla ya uwekaji wa Jiwe la Msingi la Mradi wa Maji wa Mbalache-Lupombwe.

“Kila kona ya nchi hii kuna mradi unajengwa na niwahakikishie miradi mingi inayojengwa kipindi hiki ni miradi yenye ubora mzuri na hata kwenye Mbio za Mwenge mwaka huu miradi iliyokaguliwa ilipongezwa na viongozi wa mbio za mwenge” alisema Mhandisi Sanga.

Mhandisi Sanga aliwapongeza wataalam Wizara ya Maji kwa kuhakikisha ubora wa miradi lakini pia aliwapongeza Viongozi wa Serikali na Chama cha Mapinduzi Wilayani Makete kwa jitihada zao, ufuatiliaji na usimamizi wa ujenzi wa miradi ya maji wilayani humo.

No comments:

Powered by Blogger.