LIVE STREAM ADS

Header Ads

Mtozi Alloyce Nyanda wa Star TV uso kwa uso na Balozi wa Ethiopia

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Online Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Balozi wa Ethiopia nchini Tanzania, Mhe. Balozi Shibru Mamo Kedida (kulia) amefanya mahojiano na mtangazaji wa Star TV, Mtozi Alloyce Nyanda (kushoto) kuhusu masuala mbalimbali ikiwemo mzozo unaondelea Ethiopia (Northern Part of Ethiopia) na kutoa msimamo wa Serikali ya Taifa hilo juu ya mzozo huo.

Katika mahojiani hayo yaliyofanyika jijini Dar Es salaam, Mhe. Balozi Kedida amesema Serikali ya Ethiopia inazingatia zaidi haki na Uhuru wa watu wake katika kupata maendeleo.

"Maendeleo ni haki ya kila mwanachi na ni suala la kuonyesha ni jinsi gani maendeleo ndiyo msingi mkubwa wa ustawi wa watu wetu" amesema Balozi Kedida.

Aidha mahojiano hayo yamempa fursa Balozi Kedida kutoa msimami na mtazamo juu ya ujenzi wa Bwala kubwa la kifua umeme linalojengwa nchini Ethiopia ambalo litaleta mapinduzi makubwa ya uchumi na ajira kwa wananchi wa Taifa hilo na Afrika kwa ujumla kwa kuwa ujenzi huo hauna madhara zaidi ya Faida.

Ifahamike kuwa Ethiopia imekuwa ikipata shutuma kutoka nchini Misri kwa kutumia Mto Nile kujenga bwawa la umeme ambalo Misri inadai Ethiopia haina haki kisheria kutumia maji ya Mto Nile.
Usikose kufuatilia mahojiano hayo katika kipindi cha 'The Big Ajenda' na Mtozi Alloyce Nyanda kupitia Star TV.

No comments:

Powered by Blogger.