TANESCO Mwanza watinga mitaani kutoa elimu kwa wananchi
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Online Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Katika kuadhimisha Wiki ya Elimu kwa Wateja Duniani, shirika la umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa Mwanza, limetumia fursa hiyo kwa kuwafuata mitaani wananchi ili kuwaelimisha kuhusiana na huduma mbalimbali zinazotolewa na shirika hilo.
Akizungumza Alhamisi Oktoba 06, 2022 katika mitaa mbalimbali ya Jiji la Mwanza wakati wa zoezi hilo lililoambatana na kugawa vipeperushi vya jumbe mbalimbali, Afisa Masoko Mwandamizi TANESCO Mkoa Mwanza, Flaviana Moshi aliwahimiza wateja wa shirika hilo kutumia huduma mpya ya kidijitali ya NIKONEKT ili kupata huduma mbalimbali ikiwemo kuunganishiwa umeme kwa muda mfupi.
Alisema ili mteja kunufaika na huduma hiyo anapaswa kuwa na nambari ya kitambulicho cha NIDA, kupakua programu ya NIKOTEKT, kuingia kwenye tovuti ya www.tanesco.co.tz ama kwa kupiga *152*00# ambapo baada ya kutuma maombi na kufanya malipo atapata huduma kwa muda mfupi kuanzia siku nne hadi 14.
Naye Afisa Masoko TANESCO Mkoa Mwanza, Joyce Makori alitumia fursa hiyo kutoa elimu kwa wananchi kuhusiana na matumizi sahihi na usalama wa umeme ambapo aliwatahadharisha kutochezea ama kufanya shughuli za kibiashara katika miundombinu ya TANESCO ikiwemo chini ya nyaya ama transfoma.
Kwa upande wake Afisa masoko mwingine TANESCO Mkoa Mwanza, Prisca Kayaga aliwaelimisha wananchi sababu za umeme kukatika katika baadhi ya maeneo nyakati za mchana ni kutokana na kiangazi kilichosababisha vyanzo vya maji vya kuzalisha umeme kupungua na hivyo shirika kulazimika kuzima baadhi ya mitambo muda wa mchana ili maji yajae kwenye mabwawa kwa ajili ya matumizi ya usiku.
Kayaga alisema tayari shirika limeanza mikakati ya kukabiliana na changamoto hiyo kwa kuanza utekelezaji wa miradi ya kuzalisha umeme kwa kutumia nishati ya jua pamoja na upepo. Pia aliongeza kuwa kukamilika kwa miradi mikubwa kama ya Mwalimu Nyerere na Rusumo itasaidia kuzalisha umeme wa kutosha na kuondoa kabisa changamoto hiyo.
Baadhi ya wateja akiwemo Denis Onyango walitumia fursa hiyo kuomba TANESCO kuongeza kasi ya kusambaza miundombinu ya umeme ikiwemo nguzo ili nao wanufaike na nishati ya umeme. Walisema ni ajabu baadhi ya Kata ikiwemo Kishiri na Nyamhongolo kuwa katika Jiji la Mwanza lakini mitaa yake ikakosa huduma ya umeme.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Afisa Masoko Mwandamizi TANESCO Mkoa Mwanza, Flaviana Moshi (kulia) akitoa elimu kwa mkazi wa Jiji la Mwanza kuhusiana na huduma za shirika hilo.
Afisa Masoko TANESCO Mkoa Mwanza, Johari Mrisho akiwaelimisha wananchi kuhusiana na matumizi sahihi na salama ya nishati ya umeme pamoja na kutumia mfumo wa NIKONEKT kuwasilisha maoni yao TANESCO.
Afisa Masoko TANESCO Mkoa Mwanza, Prisca Kayaga akigawa vipeperushi vyenye jumbe mbalimbali za TANESCO katika stendi ya daladala Igombe wilayani Nyamagana.
Afisa Masoko TANESCO Mkoa Mwanza, Prisca Kayaga (kulia) akimwelekeza mwananchi namna ya kujiunga na huduma ya NIKONEKT katika eneo la Kamanga jijini Mwanza.
Afisa Masoko Mwandamizi TANESCO Mkoa Mwanza, Flaviana Moshi akitoa elimu kwa umma katika eneo la stendi ya mabasi Nyamhongolo wilayani Ilemela.
Afisa Masoko TANESCO Mkoa Mwanza, Prisca Kayaga (kulia) akitoa elimu na kugawa vipeperushi kwa wananchi katika eneo la stendi ya mabasi Nyamhongolo.
Bodaboda katika eneo la Nyamhongolo pia walifikiwa na maafisa kutoka TANESCO Mkoa Mwanza.
Maafisa wa TANESCO Mkoa Mwanza wakitoa elimu kwa bodaboda kuhusiana na huduma zinazotolewa na shirika hilo pamoja na maboresho yanayoendelea kufanyika ili kuimarisha upatikanaji wa umeme.
Maafisa wa TANESCO Mkoa Mwanza wakitoa elimu kwa bodaboda kuhusiana na huduma zinazotolewa na shirika hilo.
Afisa Masoko TANESCO Mkoa Mwanza, Joyce Makori akigawa vipeperushi kwa wananchi katika eneo la stendi ya Nyamhongolo.
Afisa Masoko TANESCO Mkoa Mwanza, Prisca Kayaga akitoa elimu kuhusiana na huduma za shirika hilo katika stendi ya Nyamhongolo.
Maafisa wa TANESCO Mkoa Mwanza wakitoa elimu katika stendi ya Nyamhongolo.
Maafisa wa TANESCO Mkoa Mwanza wakitoa elimu katika stendi ya Nyamhongolo.
SOMA>>> Habari zaidi hapa
No comments: