LIVE STREAM ADS

Header Ads

Waziri Bashe asisitiza wakulima kujisajili

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Online Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Wakulima nchini wametakiwa kujisajili kwenye mfumo wa ruzuku ili kupata namba ya siri itakayowasaidia kununua mbolea kwa bei elekezi iliyotangazwa na Serikali.

Rai hiyo ilitolewa Jumatatu Oktoba 17,2022 na Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe wakati akifungua maadhimisho ya siku ya kimataifa ya vyama vya ushirika wa akiba na mikopo duniani yaliyofanyika kitaifa kwenye viwanja vya Furahisha mkoani Mwanza.

Alisema anafahumu kuna changamoto ya mawakala wa kuuza mbolea katika baadhi ya maeneo na Serikali iko kwenye hatua za mwisho za kuongeza idadi ya mawakala kwenye maeneo ambayo yanaupungufu ili wakulima waweze kupata huduma ya kununua mbolea kwa ukaribu.

"Namba ya siri ndio silaha yako ukiitoa kwa mtu mwingine anaweza kununua mbolea kupitia namba yako hiyo nawewe ukapoteza fursa ya kuinunua mbolea ya ruzuku" alisema Bashe.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Muungano wa vyama vya Ushirika vya Akiba na Mikopo (SCCULT), Dkt.Cuthbert Msuya alisema lengo ya maadhimisho hayo ni kuwakumbuka na kuwaenzi waasisi wa ushirika wa akiba na mikopo kwa mchango wao mkubwa wa kueneza dhana ya ushirika pamoja na kuthamini mchango mkubwa wa vyama vya ushirika wa akiba na mikopo katika kukuza na kuimarisha uchumi wa nchi mbalimbali duniani.

Msuya aloeleza kuwa katika uendeshaji wa SACCOS nchini, mafanikio mbalimbali yamepatikana ambayo ni kutengeneza fursa za uwekaji akiba kwa wanachama, ukopaji kwa mashariti nafuu, ufikishaji wa huduma za kifedha katika maeneo ambayo taasisi nyingi za kifedha hazifiki na fursa za uwekezaji, maendeleo na masuala mbalimbali ya kijamii.

Kauli mbiu ya mwaka huu ni kwenye maadhimisho hayo ni "imarisha uwezo wako wa kifedha wa siku zijazo kupitia ushirika wa akiba na mikopo" 
Na Hellen Mtereko, Mwanza
Mwenyekiti wa Bodi ya SCCULT, Dkt. Cuthbert Msuya akizungumza kwenye Maadhimisho ya siku ya kimataifa ya vyama vya ushirika wa akiba na mikopo duniani yaliyofanyika kitaifa mkoani Mwanza.
Washiriki kutoka vyama mbalimbali vya ushirika wakiwa kwenye maadhimisho hayo.

No comments:

Powered by Blogger.