LIVE STREAM ADS

Header Ads

Wananchi wahimizwa kubadili mtindo wa maisha, kuepuka magonjwa yasiyoambukiza

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Online Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Wananchi wamehimizwa kubadili mtindo wa maisha ikiwemo kuzingatia mlo wa vyakula vyenye lishe bora na kufanya mazoezi ili kujiepusha na magonjwa yasiyoambukiza yakiwemo ya moyo, kisukari na saratani.

Rai hiyo imetolewa Jumamosi Novemba 12, 2022 na Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza, Mhandisi Elikana Balandya wakati akihitimisha Maadhimisho ya Wiki ya Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa Yasiyoambukiza iliyofanyika kitaifa uwanja wa CCM Kirumba.

Amesema magonjwa yasiyoambukiza ambayo husababishwa na ulaji usiofaa na tabia bwete/ kutofanya mazoezi yamekuwa yakididimiza nguvu kazi ya taifa kwa kusababisha vifo ambapo kati ya vifo 100, vifo 33 husababishwa na magonjwa yasiyoambukiza huku takwimu duniani zikioneshwa watu milioni 41 walipoteza maisha mwaka 2022/23.

“Ni lazima juhudi ziendelee kufanyika kupambana na magonjwa yasiyoambukiza, elimu iendelee kutolewa kwa jamii kuepuka ulaji usiofaa kama vyakula vyenye mafuta mengi, chumvi na sukari nyingi" amesema Balandya akiwahimiza wananchi kuzingatia elimu waliyoipata kwenye maadhimisho hayo.

Balandya pia amewahimiza wananchi kuwa na utamaduni wa kupima afya mara kwa mara hatua inayosaidia kubaini dalili za awali za magonjwa yasiyoambukiza na kuanza matibabu mapema badala ya kusubiri hadi waugue kwani ugonjwa unakuwa kwenye hatua mbaya.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Huduma za Tiba kutoka Wizara ya Afya, Prof. Paschal Ruggajo amesema katika maadhimisho hayo kulikuwa na utoaji bure huduma mbalimbali kwa wananchi ikiwemo upimaji wa magonjwa ya moyo, saratani, kisukari, kinywa na meno pamoja na utoaji chanjo ya UVIKO-19 ambapo hadi jana wananchi 1,428 walikuwa wamehudumiwa.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ukimwi, Kifua Kikuu, Dawa za Kulevya na Magonjwa Yasiyoambukiza, Fatma Tawfiq Kamati hiyo itaendelea kuishauri vyema Serikali ili kuhakikisha inaongeza bajeti itakayosaidia kupambana na magonjwa yasiyoambukiza.

Huu ni mwaka wa nne Tanzania kuadhimisho ya Wiki ya Kuzuia na Kudhibiti Magonjwa Yasiyoambukiza na yameambatana na kaulimbiu isemayo "Badili Mtindo wa Maisha, Boresha Afya" ikihamasisha wananchi kuzingatia mtindo bora wa maisha ikiwemo ulaji wa vyakula lishe na kuzingatia mazoezi.

Mgeni rasmi kwenye kilele cha maadhimisho hayo alikuwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ambaye ameshindwa kufika kutokana na mwingiliano wa majukumu.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza, Mhandisi Elikana Balandya akizungumza kwenye kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa Yasiyoambukiza yaliyofanyika kitaifa jijini Mwanza.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza, Mhandisi Elikana Balandya akizungumza kwenye kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa Yasiyoambukiza.
Mkurugenzi wa Huduma za Tiba kutoka Wizara ya Afya, Prof. Paschal Ruggajo (katikati) akiwa na viongozi mbalimbali kwenye kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa Yasiyoambukiza.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza, Mhandisi Elikana Balandya tuzo kwa wadau waliofanikisha maadhimisho hayo.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza, Mhandisi Elikana Balandya tuzo kwa wadau waliofanikisha maadhimisho hayo.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza, Mhandisi Elikana Balandya tuzo kwa wadau waliofanikisha maadhimisho hayo.
Wadau waliofanikisha maadhimisho hayo wamekabidhiwa tuzo huku washiriki wa mashindano mbalimbali ikiwemo kuendesha baiskeli wakikabidhiwa zawadi.
Wadau mbalimbali wakiwa kwenye maadhimisho hayo.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.