PICHA: Kilele cha Wiki ya Magonjwa Yasiyoambukiza
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Online Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Fuatilia matukio mbalimbali katika picha kwenye kilele cha maadhimisho ya nne ya Wiki ya Kuzuia na Kudhibiti Magonjwa Yasiyoambukiza yaliyoanza Novemba 05-12, 2022 jijini Mwanza.
Maadhimisho hayo yaliambatana na utoaji huduma za afya bure ikiwemo kupima magonjwa mbalimbali yasiyoambukiza kama vile presha, kisukari, macho, saratani, kinywa na meno pamoja na utoaji wa chanjo ya UVIKO 19.
Pia kulikuwa na michezo mbalimbali ikiwemo jogging, baiskeli, mpira wa Pete na mpira wa miguu kama sehemu ya kuhamasisha jamii kufanya mazoezi ili kujikinga na magonjwa yasiyoambukiza.
Magonjwa yasiyoambukiza ni miongoni mwa sababu za ongezeko la vifo nchini kwani inaelezwa kuwa kila vifo 100, vifo 33 vinatokana na magonjwa hayo, hivyo wananchi wanahimizwa kuwa na utamaduni wa kupima afya mara kwa mara ili kutambua hali yao kiafya hatua inayosaidia kuanza matibabu mapema mgonjwa anapobainika kuwa na dalili za magonjwa hayo.
Kitaifa maadhimisho ya Wiki ya Kuzuia na Kudhibiti Magonjwa Yasiyoambukiza mwaka huu 2022 yamefanyika katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza yakiambatana na kaulimbiu "Badili Mtindo wa Maisha, Boresha Afya" ikihamasisha wananchi kuzingatia mtindo bora wa maisha ikiwemo ulaji wa vyakula lishe na kuzingatia mazoezi.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
No comments: