LIVE STREAM ADS

Header Ads

TGNP yafanya Tathmini ya matokeo ya kukua kwa Tapo la Ufeminia ngazi ya jamii

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Online Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com

Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Lilian Liundi akizungumza

Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Lilian Liundi 

Na Deogratius Temba

Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) umewakutanisha washiriki 30, wawakilishi wa mashirika na vikundi kutoka mikoa tisa ya mradi wa Ujenzi wa TAPO la Ukombozi wa wanawake  na uimarishaji wa harakati za kupigania Haki za wanawake na usawa wa Kijinsia nchini Tanzania.

Mradi huu unaojulikana kama  “Sauti za Wanawake na Uongozi” unaofadhiliwa na Ubalozi wa Canada (GAC) unalenga kuhakikisha kila mwanajamii anatambua umuhimu wa haki za wanawake, usawa wa Kijinsia na kusimamia misingi ya Haki na Usawa wa Kijinsia katika utendaji wa kila siku katika jamii. 

Warsha ya siku mbili (2)  inayofanyika katika Ofisi za TGNP, imejikita katika kuvuna matokeo ya mafunzo ya ufeminia waliyopatiwa hapo awali kwa lengo la kutambua michango ya mashirika mbalimbali na vikundi katika kuendeleza na kuimarisha vuguvugu la utetezi wa haki za wanawake.Akizungumza wakati wa ufunguzi wa warsha hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Lilian Liundi, amesema kwamba mradi huo unalenga kuhakikisha vuguvugu la harakati za kutetea Haki za wanawake na usawa wa Kijinsia linasambaa,  ili jamii yote izingatie msingi ya usawa wa kijinsia. 

“Tunatamani kuona kila mtu katika taifa letu akiwa na uelewa wa masuala ya usawa wa kijinsia na kuhsehimu haki za binadamu. Nyie ambao mnatokea kwenye taasisi na vikundi mbalimbali katika ngazi ya jamii, ndio mmepewa jukumu la kusambaza hii elimu na kubadilisha mtazamo wa jamii kuhusu usawa wa Kijinsia na Haki za wanawake. Tunategemea kuona mabadiliko makubwa sana huko mlinakotokea” alisema Liundi



No comments:

Powered by Blogger.