LIVE STREAM ADS

Header Ads

Shirika la KIVULINI laendesha mdahalo kwa Wanawake Soko la Mirongo Mwanza

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Shirika la kutetea haki za watoto na wanawake la KIVULINI limeendesha mdahalo kwa wanawake wajasiriamali katika soko la Mirongo jijini Mwanza, kwa lengo la kuwajengea uelewa kuhusu namna ya kuzuia na kujiepusha na vitendo vya ukatili wa kijinsia.

Mdahalo huo umefanyika Jumanne Novemba 29, 2022 ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia duniani yaliyoanza Novemba 25, 2022 yakitarajiwa kufikia tmati Disemba 10, 2022.

Akizungumza kwenye mdahalo huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la KIVULINI, Yassin Ally amewahimiza kuimarisha mahusiano na malezi bora katika familia hatua itakayosaidia kutokomeza vitendo vya ukatili wa kijinsia katika jamii hususani kwa watoto na wanawake.

Ally amesema kukosekana kwa malezi bora katika familia, wazazi na walezi kukosa muda wa kufuatilia mienendo ya watoto wao kumechochea ongezeko la matukio ya ukatili ikiwemo ubakaji na ulawiti kwa watoto na hivyo kuwakumbusha wanawake walioshiriki mdahalo huo kutambua wajibu wao.

"Takwimu za jeshi la polisi kuanzia mwezi Januari hadi Septemba mwaka huu 2022 zinaonesha watoto 1,044 wamelawitia, hiyo ni ishara tosha wazazi wakiwemo wanawake hawana muda wa kufuatilia usalama wa watoto wao" amesema Ally.

Akichangia hoja kwenye mdahalo huo, mjasiriamali Pili Mwita amesema wanawake wakijitambua na kushirikiana vyema na waume zao kulea watoto watasaidia kupunguza matukio ya ukatili wa kijinsia ambayo yamekuwa yakiripotiwa katika maeneo mbalimbali nchini.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mkurugenzi Mtendaji Shirika la KIVULINI, Yassin Ally akiwasilisha mada wakati wa mdahalo kwa wanawake wajasiriamali katika soko la Mirongo jijini Mwanza.
Wanawake wajasiriamali soko la Mirongo jijini Mwanza wakifuatilia mada kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la KIVULINI, Yassin Ally (kulia).
Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa Mwanza, Isack Ndasa akizungumza kwenye mdahalo huo ambapo amewataka wanawake kutonyamazia vitendo vya ukatili wa kijinsia.
Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa Mwanza, Isack Ndasa akizungumza kwenye mdahalo wa kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia uliofanyika katika soko la Mirongo jijini Mwanza.
Mmoja wa wanawake wajasiriamali katika soko la Mirongo jijini Mwanza, Pili Mwita akichangia hoja kwenye mdahalo huo.
Mjasiriamali katika soko la Mirongo jijini Mwanza, Shamsa Ibrahim akichangia hoja kwenye mdahalo huo.
Mjasiriamali Leah Getman akizungumza kwenye mdahalo huo.
Mjasiriamali Suzana Bugume akichangia mada kwenye mdahalo huo.
Mwanamama Happy Misana akichangia mdahalo huo.
Mwelimishaji rika, Radhaman Yassin akichangia hoja kwenye mdahalo huo.
Akina mama wajasiriamali soko la Mirongo jijini Mwanza wakifurahia burudani wakati wa mdahalo huo.

No comments:

Powered by Blogger.