LIVE STREAM ADS

Header Ads

UTPC yaendesha mdahalo kwa waandishi wa habari vijana

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Online Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) kwa kushirikiana na Taasisi ya International Media Support (IMS), umefanya mdahalo wa Uhuru wa Kujieleza na Haki ya Kupata Taarifa kwa Waandishi wa Habari Vijana.

Mdahalo huo umefanyika Jumatatu Novemba 21, 2022 katika Hoteli ya Gold Crest jijini Mwanza na kuhudhuriwa na waandishi wa habari vijana walio kazini ambao ni wanachama wa MPC pamoja na wanafunzi wa uandishi wa habari kutoka Chuo Kikuu Cha Mtakatifu Agustino (SAUT).

Akifungua mdahalo huo, Mjumbe wa Bodi ya UTPC, Paulina David amewaasa waandishi wa habari vijana kuitumia vizuri mitandao ya kijamii kwa kuandika maudhuri yanayozingatia weledi kwani mchango wao ni mkubwa katika kuelimisha umma.

"Ukali wa Sheria za Habari ni kikwazo katika kurahisisha upatikanaji wa taarifa na kuhabarisha wananchi hususani kupitia Habari za Uchunguzi" ameeleza Paulina.
"Hii fursa ya kujadiliana na Serikali kupitia kwa Waziri wa Habari, Nape Nnauye kuhusu marekebisho ya Sheria ya Huduma za Habari ya mwaka 2016 tunapaswa kuitumia vizuri kwani hatutaipata tena tukiitumia vibaya" ameeleza Afisa Programu UTPC, Victor Maleko.
"Vyombo vya Habari Tanzania vimetoka jehanamu katika kipindi cha miaka miwili ya utawala wa Rais Samia Suluhu Hassan. Tunaamini mazungumzo yanayoendelea yatatufikisha peponi" amesema Mwenyekiti wa MPC, Edwin Soko.
"Uhuru wa kutafuta, kupokea na kusambaza taarifa si hisani, ni haki ya kila mtu kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ibara ya 18. Vijana tumieni haki hiyo kutengeneza Maudhui yenye kuleta mabadiliko katika jamii na kuyasambaza kupitia mitandao ya kijamii" Ameeleza Mhadhiri Msaidizi Chuo Kikuu SAUT, Martin Nyoni.
Washiriki wakifuatilia mdahalo huo.
Washiriki wakifuatilia mdahalo huo.
Washiriki wakiwa kwenye mdahalo huo.

No comments:

Powered by Blogger.