LIVE STREAM ADS

Header Ads

Uhaba wa Mvua za Vuli ukanda wa Pwani unavyosababisha mfumko wa bei na uhaba wa chakula

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Online Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Bwana James Bitungwanayo Mkulima akiwa katika Shamba lake ambalo halijalimwa kutoka na kukosekana kwa mvua za vuli. ***

“Tanzania sio nchi ya kulalamika kuhusu chakula,Tanzania inapaswa kuwa nchi ya kulisha Chakula Nchi zingine” Lucas Malembo Mkurungenzi Mtendaji Malembo Farm


Na Seleman Mahinya

Kwa miaka mitatu iliyopita nchi nyingi duniani, Tanzania ikiwemo zimeshuhudia ugumu wa maisha uliotokana mfumuko wa bei za bidhaa muhimu kwa binadamu, bidhaa vya vyakula. Kwa kiasi kikubwa mfumuko huo uliochangiwa na athari za UVIKO-19 kwa miaka 2019 mpaka 2021 na baadae ni athari ya vita vya Urusi na Ukraine ambayo ilizuka mwezi februari mwaka 2022.


Lakini bado nafuu juu ya kushuka kwa bei za bidhaa hizo muhimu kwa binadamu na hii inatokana na jamii ya afrika mashariki ikiwemo Tanzania kushuhusia mabadiliko vya hali ya hali ya hewa .


”Kipindi kama hiki miaka iliyopita ni kipindi cha kulima watu unawakuta wapo 'busy' kulima lakini kwa sasa hivi nikama  mnavyoona hali ni ngumu ukame ni mwingi, mvua hamna, mito imekauka hali si nzuri kiufupi”anasema Bwana James Mkazi wa kijiji cha Konga wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro.

Mamlaka ya hali ya hewa nchi TMA mwezi septemba ulitoa taarifa ya uchambuzi wa mwenendo wa mifumo ya hali ya hewa na mwelekeo wa msimu wa mvua za Vuli kipindi cha Oktoba - Disemba 2022, ambao ulilenga kutoab ushauri na tahadhari kwa wadau wa sekta mbalimbali kama vile kilimo na usalama wa chakula, mifugo na uvuvi, maliasili, wanyama pori na utalii, nishati na maji, usafirishaji (nchi kavu, kwenye maji na angani), mamlaka za miji, afya pamoja na menejimenti za maafa. Utabiri huo ulikuwa ni mahsusi kwa maeneo yanayopata misimu miwili ya mvua kwa mwaka (Nyanda za juu kaskazini mashariki, Pwani ya kaskazini, Ukanda wa Ziwa Viktoria pamoja na kaskazini mwa mkoa wa Kigoma). 


 “Kwa kipindi hiki tunatarajia mvua hizi kuwa chini ya kiwango kwa mikoa ya ukanda  pwani”

Amesema Joyce Mwakwata Mtaalamu na Mchambuzi wa Masuala ya Utabiri wa hali ya hewa kutoka Mamlaka ya hali ya hewa nchini (TMA).

Bi. Joyce Makwata akichambua taarifa ya mwenendo wa mvua za mvuli kwa mikoa ya Dar es salaam.

Gasper Kigere ni Mkulima wa Mazao ya chakula kijiji cha Tangeni wilayani Mvomero Mkoani Morogoro ,Gasper anasema amekuwa akijishughulisha na kilimo kwa zaidi ya miaka kumi mkoani humo huku akieleza namna mvua za vuli vinavyowasaida katika shughuli za kilimo na kupungua kwake kunavyopelekea kupata mazao finyu.


“Utofauti pindi mvua za vuli zikiwahi takribani kama mwezi wa kumi huu huwa tunapata mvua za vuli mazao yanakuwa yanapendeza yanastawi kwa uzuri zaidi na kivuno kinakuwa vizuri tofauti na hivi kunavyokuwa na ukame, kunapokuwa na ukame kilimo akileti kivuno zinazotakiwa” 

Anasema Gasper huku akiongeza kuwa katika kipindi hiki ambacho kunakuwa na uhaba wa mvua za vuli huwa wanahamishia shughuli zake mabondeni kwa huko anaweza kuchimba visima vya muda ili kupata maji kwa ajili ya mazao yake shambani.


“Huwa tunachukua tahadhari kipindi cha mabadiliko ya hali ya hewa yanapotokea hata mito na vyanzo vya maji vinakauka ,kwahiyo kwa sisi wakulima huwa tunatafuta mashamba yaliyokuwa bondeni  ambayo unaweza ukaanda miundombinu ya maji michache kwa ajili ya mazao machache kwa maji machache yatakayopatikana kwenye mazingira hayo haswa huwa tunachimba visima vidogo vidogo ambavyo msimu wa masika ukija huwa vinajifukia”  ameongeza Gasper.

Pamoja na athari hizo zilizotajwa za kukosekana kwa mvua za vuli kwa mkoa wa Morogoro lakini katika mwa shida hii kuna baadhi ya wakulima wamejitahidi kuwekeza kwenye njia mbadala za kuweza kukabiliana na shida hii ya kukosekana na mvua za mvuli.

Maua Elikana ni Mkulima katika kijiji cha tangeni Mvomero yeye aliamua kuwekeza kwenye kukodisha mashine ya kuvuta Maji na kuajiri vijana watanaomsaidia kumwagilia shambani kwake.


“Kipindi kama hiki ambacho kun akuwa mvua za vuli hazipo huwa natumia vijana kunyeshea kwa kutumia mipira inakuwa nin gharama kwa sababu unanunua mafuta bado vijana wale haujawalipa kwahiyo gharama inakuwa ni kubwa ,kwa wiki unatakiwa kunyesea mara mbili”anasema Bi Maua huku akiongeza kuwa si kila mkulima yupo kwenye nafasi ya  kumudu gharama za kuajiri watu wa kumwagili na kukodisha mashine za kuvuta maji shambani.


“Si kila mtu ana nafasi ya kuweza kuajiri watu na kun awatu wanashindwa wanaamua kuacha kuendelea na kilimo” anaongeza Bi. Maua.

Bi. Maua Elikana akikagua shamba lake kabla ya kuanza shughuli ya umwagiliaji.

Mmoja ya wafanyakazi wa Bi Maua akitekeleza majukumu ya kuwangilia shamba. Kwa miezi hivi karibuni kuanzia mwezi Septemba mpaka Novemba kiujumla bei ya vyakula nchini imekuwa ikipanda mathali kwa Mwezi Septemba kulikuwa na asilimia 4.8% na mwezi Oktoba ulizidi kupanda mpaka kufikia Asilimia 4.9%.

Mkoa wa Dar es salaam kwa kiasi kikubwa wenye wakazi Milioni 5.3  unategemea chakula kutoka mikoa mingine na Morogoro ni moja ya mikoa inayolisha Dar es salaam kwa kiasi kikubwa. Katika jedwali hapo juu linaonesha na mfumuko wa mazao ya Mahindi, maharage na mchele kwa miezi mitatu iliyopita.


Mtaalamu na mshauri wa masuala ya kilimo nchini Bwana Lucas Malembo ambaye ni mkurugenzi wa kampuni ya Malembo Farm inayojihusisha na ushauri juu ya masuala ya kilimo anasema bado kuna nafasi ya kuendelea kufanya kilimo kwa wakulima wa hali ya chini ambao hawazezi kumudu gharama ya kujihusisha na kilimo cha umwagiliaji.


“Yapo mazao ambayo wataalamu tumekuwa tukishauri wananchi wawe wanashiriki ili kupunguza hayo makali ya ukame, Mazao kama viazi utamu yanastahimili ukame , Mazao kama mihogo yanastahimili ukame ,Mazao kama mtama  yanastahimili ukame ni baadhi ya mazao yanayolimika ukanda wetu huu wa pwani kwahiyo ni mazao ambayo wananchi wanaweza kushiriki kuyalima ” anasema Bwana Lucas Malembo.

Serikali kupitia waziri wa wizara ya Kilimo Hussein Bashe anakirin kuwa kama nchi tunapitia changamoto ya mabadiliko ya tabia ya nchi amabayo kwa kiasi kikubwa yanaathiri shughuli za kilimo lakini kama serikali wamejipanga kuhakikisha shughuli za kilimo zinaendelea  hata katika vipindi ambavyo mvua zinakuwa zinasusua kunyesha.


“Serikali imeongeza fedha na tumeanza kuchukua hatua , tuna ekari jumla ya milioni ishirini na tisa zinazofaa kwa umwagiliaji lakini huko nyuma tumekuwa tukijenga miundombinu ambayo iansubiri na wenyewe kudra za mwenyezi Mungu mvua inyeshe ili watu waweze kutumia hiyo miundombinu” alisema Mhe. Bashe wakati akijibu maswali bungeni mapema mwezi novemba,2022.


Pia ameongeza kusema kuwa “Kwa mwaka huu wa fedha tutajenga mabwawa 23 na niwatoe hofu wabunge na kamati ya bajeti, hatua ya serikali kujenga mabwawa maeneo ya kati sio hatua ya kutilia mashaka ni hatua iliyofanyiwa utafiti wa kisayansi na kujiridhilisha”.

Bwana Malembo anasema njia ya kudumu ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi ni kuhakikisha jamii inakuwa na uelewa wa namna ya kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa hivyo wamewataka wa  Wadau wa mazingira na kilimo kuhakikisha wanaeneza elimu  kwa wananchi juu ya namna ya kulinda na kutunza mazingira ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi.


“Lazima tuwe na kampeni itakayosaidia kuwaelewesha jamii uelewa bado ni mdogo pengine watu hatujui kama pengine kutupa tu kopo , kutupa uchafu wako nje kuwa ni moja ya njia ambayo ina hatarisha mazingira tuliyonayo ,kwahiyo tuna kila sababu ya tuoa elimu tuanzie misikitini ,tuanzie makanisani sisi kwenye makazi yetu kila mtu aliye na familia aliye na marafiki maana ya mabadiliko ya tabia ya nchi na athari zake ni nini” amesema Malembo.


Lakini rais wa jamhuri wa Muungano wa Tanza nia Samia Suluhu Hassan aliwatoa hofu wananchi juu ya usalama wa chakula nchini kwani kuna tani laki moja na nusu kwa ajili ya kuikwamua nchi iwapo itapitia katika ugumu wowote.


“Tuna tani zisizo pungua laki mmoja na nusu ambazo tumeziweka kwa ajili ya  wakati wa magumu|” alisema rais Samia Suluhu  wakati akihutubia  katika jubilee ya miaka 50 ya tangu kunanzishwa kwa umoja wa wanawake wakatoliki Tanzania (WAWATA) Sherehe hizo zilizofanyika uwanja wa Benjamini Mkapa  tarehe 11 Septemba 2022.

Rais Samia Suluhu Hassan akizungumzia usalama wa chakula nchini.

No comments:

Powered by Blogger.