LIVE STREAM ADS

Header Ads

Wanafunzi wakumbushwa kujiepusha na ngono zembe vyuoni

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Online Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Wanafunzi wa vyuo vya kati na vyuo vikuu nchini wametakiwa kujiepusha na ngono zembe kwa kuwa hatua hiyo inawaweka kwenye hatari ya kupata magonjwa ya zinaa huku wakishindwa kutimiza malengo yao kielimu.

Rais hiyo imetolewa na Novemba 19, 2022 na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la kutetea haki za wanawake na watoto KIVULINI, Yassin Ally wakati akitoa semina kuhusu stadi za kujitambua kwa wanafunzi wa Taasisi ya Teknolojia Dar es salaam (DIT) tawi la Mwanza.

Yassin amesema imeibuka tabia ya wanafunzi wa vyuo vya kati na vyuo vikuu nchini kujiingiza katika mahusiano na wapenzi wengi kutokana na uhuru uliopitiliza na hivyo kujikuta wakiangukia mikononi mwa matapeli wa mapenzi hatua inayowaathiri kisaiklojia na kimasomo pia.

"Imeibuka kozi isiyotambulika inayoitwa 'Boyfriend and girlfriend Management', inawapotezea malengo wanafunzi vyuoni. Wanatumia fedha za kujikimu kwa ajili ya kuwekeza kwenye mahusiano na athari zake ikitokea usaliti, wanaathirika kisaikolojia na kushindwa kuzingatia masomo" alionya Yassin.

Yassin ametumia fursa hiyo kutoa rai kwa wakuu wa vyuo nchini kutoa mwongozo wa semina elekezi zitakazokuwa zinatolewa mara kwa mara kwa wanafunzi ili kuwajengea uwezo na stadi za kujitambua, kujiwekea malengo, kujilinda na kujiepusha na vishawishi vinavyoweza kuwasababishia madhara ikiwemo ukatili wa kingono.

Mkurugenzi wa Chuo cha DIT Tawi la Mwanza, Dkt. Alber Mmari alisema chuo hicho kimekuwa na utaratibu wa kutoa semina elekezi ili kuwasaidia wanafunzi wa chuo hicho kupata mbinu za kujikinga na vishawishi mbalimbali ikiwemo vya kimapenzi hatua inayowasaidia kuzingatia masomo.

Naye Rais wa Jumuiya ya Wanafunzi DIT Tawi la Mwanza, Sharifa Abubakari amesema mahusiano ya mapema kwa wanafunzi vyuoni ni kikwazo kinachowakwamisha kimasomo na hivyo kuwahimiza kuzingatia lengo lao lao kuu ambalo ni masomo.

Kwa upande wake Naibu Kamishna wa Jinsia na Maendeleo ya Wanawake TAHLISO, Hawa Issa amewahimiza wanafunzi wa vyuo kujiwekea malengo na kuhakikisha wanayatimiza huku suala la mapenzi wakiliweka kando kwanza hadi wakati mwafaka unapowadia.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mkurugenzi Mtendaji Shirika la KIVULINI, Yassin Ally akitoa semina kwa wanafunzi wa Chuo cha DIT Tawi la Mwanza.
Wanafunzi wa Chuo cha DIT Tawi la Mwanza wakifuatilia mada kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la KIVULINI, Yassin Ally (kulia).
Mkurugenzi Mtendaji Shirika la KIVULINI, Yassin Ally (kushoto) akitoa semina kwa wanafunzi wa DIT tawi la Mwanza.
Mkurugenzi wa Chuo cha DIT Tawi la Mwanza, Dkt. Alber Mmari akizungumza wakati wa semina hiyo.
Mkurugenzi wa Chuo cha DIT Tawi la Mwanza, Dkt. Alber Mmari akizungumza wakati wa semina hilo.
Rais wa Jumuiya ya Wanafunzi DIT Tawi la Mwanza, Sharifa Abubakari akizungumza wakati wa semina hiyo.
Mwanafunzi wa Chuo cha DIT Tawi la Mwanza, Kassim Abdul akichangia mada kwenye semina hiyo.
Mwanafunzi wa Chuo cha DIT Tawi la Mwanza, Peter Lenard akieleza madhara ya wanafunzi kujiingiza kwenye mahusiano ya kimapenzi.
Mwanafunzi wa Chuo cha DIT Tawi la Mwanza, Francis Makono akizungumza kwenye semina hiyo.
Mwanafunzi wa Chuo cha DIT Tawi la Mwanza, Mwanaheri Juma akichangia mada kwenye semina hiyo.
Mwanafunzi wa Chuo cha DIT Tawi la Mwanza, Esther Francis akizungumza kwenye semina hiyo.
Wanafunzi wa DIT Tawi la Mwanza wakifuatilia mada wakati wa semina hiyo.
Wanafunzi wa DIT Tawi la Mwanza wakifurahia mada.
Wanafunzi wa DIT Tawi la Mwanza wakifurahia mada wakati wa semina hiyo.

No comments:

Powered by Blogger.