LIVE STREAM ADS

Header Ads

TRA yatoa msaada wa Mmatanki ya maji Hospitali mpya ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Online Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Kamishna wa Kodi za Ndani TRA, Herbert Kabyemela (kushoto)  akishikana mkono na Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga Dkt. John Luzila wakati wa kukabidhi Matanki ya Maji kwa ajili ya Hospitali hiyo.
Kamishna wa Kodi za Ndani TRA, Herbert Kabyemela (kushoto)  akishikana mkono na Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga Dkt. John Luzila wakati wa kukabidhi Matanki ya Maji kwa ajili ya Hospitali hiyo.

Na Kadama Malunde -  Malunde 1 blog 
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imekabidhi matanki mawili ya kuhifadhia maji yenye ujazo wa lita 20,000 katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga iliyopo Mwawaza katika Manispaa ya Shinyanga ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Shukrani kwa Mlipa Kodi "Asante kwa kulipa kodi kwa ustawi wa jamii na maendeleo ya taifa;Kazi Iendelee". 

Matanki hayo yamekabidhiwa leo Alhamisi Novemba 24,2022 na Kamishna wa Kodi za Ndani TRA, Herbert Kabyemela kwa Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga Dkt. John Luzila katika hospitali hiyo.

Akizungumza wakati wa kukabidhi matanki hayo mawili yenye ujazo wa lita 10,000 kila moja, Kamishna wa Kodi za Ndani TRA, Herbert Kabyemela amesema TRA imetoa matanki hayo ikiwa ni sehemu ya shukrani kwa walipa kodi ili kupunguza changamoto ya vifaa vya kutunzia maji katika hospitali mpya ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga.

“Sisi TRA tupo katika wiki ya shukrani kwa mlipa kodi iliyoanza Novemba 23 hadi Novemba 25,2022. Tumeleta matanki haya ili kupunguza changamoto ya vifaa vya kutunzia maji kwenye hospitali hii ya Rufaa mkoa wa Shinyanga”,amesema Kabyemela.

Akipokea matanki hayo, Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga Dkt. John Luzila ameishukuru TRA kwa kuikumbuka hospitali hiyo mpya na kuipatia matanki ya kuhifadhia maji akibainisha kuwa hospitali hiyo inahitaji maji kila wakati.

“TRA mmefanya jambo jema kuleta matanki ya kuhifadhia maji, hili ni jambo muhimu sana kwa sababu tunahitaji maji kila wakati kwa ajili ya huduma mbalimbali katika hospitali hii mpya ambayo imeanza kufanya kazi hivi karibuni hapa Mwawaza”,amesema Dkt. Luzila.
Kamishna wa Kodi za Ndani TRA, Herbert Kabyemela (kwenye suti katikati) akizungumza wakati wa kukabidhi Matanki ya Maji kwa Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga Dkt. John Luzila leo Alhamisi Novemba 24,2022. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Kamishna wa Kodi za Ndani TRA, Herbert Kabyemela (kwenye suti katikati) akizungumza wakati wa kukabidhi Matanki ya Maji kwa Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga Dkt. John Luzila leo Alhamisi Novemba 24,2022.
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga Dkt. John Luzila akizungumza wakati akipokea Matanki ya Maji  yaliyotolewa na TRA kwa ajili ya Hospitali hiyo. Kushoto ni Kamishna wa Kodi za Ndani TRA, Herbert Kabyemela.
Kamishna wa Kodi za Ndani TRA, Herbert Kabyemela akizungumza wakati wa kukabidhi Matanki ya Maji kwa ajili ya Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga.
Meneja wa TRA Mkoa wa Shinyanga, Faustine Mdesa (wa sita kulia) akizungumza wakati wa kukabidhi Matanki ya Maji kwa ajili ya Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga.
Muonekano wa Matanki ya Maji  yaliyotolewa na TRA kwa ajili ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga iliyopo Mwawaza Manispaa ya Shinyanga.
Muonekano wa Matanki ya Maji  yaliyotolewa na TRA kwa ajili ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga iliyopo Mwawaza Manispaa ya Shinyanga.
Muonekano wa Matanki ya Maji  yaliyotolewa na TRA kwa ajili ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga iliyopo Mwawaza Manispaa ya Shinyanga.
Muonekano sehemu ya mbele moja ya majengo ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga iliyopo Mwawaza Manispaa ya Shinyanga.

No comments:

Powered by Blogger.