LIVE STREAM ADS

Header Ads

PICHA: Mdahalo kuhusu uzoefu wa miaka 40 ya Chuo cha Maendeleo ya Jamii Ufundi Misungwi (CDTTI) Mwanza

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii Ufundi (CDTTI) Misungwi mkoani Mwanza, Arch. Charles Achuodho akitoa neno la ufunguzi kwenye mdahalo wa wazi kuhusu uzoefu wa miaka 40 tangu kuanzishwa Chuo hicho na ushirikishaji jamii pamoja na ukatili wa kijamii unaofanyika Disemba 07, 2022.
Wanafunzi wa Shule Maalum ya Mitindo wilayani Misungwi wakitumbuiza kwenye mdahalo huo.
Watumishi wa Chuo cha CDTTI Misungwi wakiwa ukumbini na washiriki wengine wa mdahalo huo unaolenga uzoefu wa miaka 40 ya Chuo hicho katika ushirikishaji jamii pamoja na elimu kuhusu masuala ya ukatili wa kijinsia. 
Washiriki wa mdahalo huo ambao unarushwa Mubashara YouTube kupitia BMG TV wakimsikiliza Mkuu wa Chuo cha CDTTI Misungwi, Arch. Charles Achuodho.
Viongozi mbalimbali walioshiriki mdahalo huo akiwemo Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Jamii kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Neema Ndoboka (wa pili kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji Shirika la KIVULINI (wa pili kulia).
Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii (CDTTI) Misungwiz Arch. Charles Achuodho akizungumza kwenye mdahalo huo.
Washiriki wakifuatilia mdahalo huo.
Wanafunzi kutoka Shule jirani na Chuo Cha CDTTI Misungwi pia wameshiriki mdahalo huo.
Mkuu wa Chuo cha CDTTI Mstaafu (katikati) akiwasili ukumbini kushiriki mdahalo kuhusu uzoefu wa miaka 40 ya Chuo hicho pamoja na elimu ya Kuzuia vitendo vya ukatili wa kijinsia.
Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maendeleo ya Jamii kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Neema Ndoboka akizungumza kwenye mdahalo huo.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Misungwi mkoani Mwanza, Kashinje Machibya akizungumza kwenye mdahalo huo.
Mwenyekiti wa SMAUJATA Taifa akichangua mada kuhusu mbinu za Kuzuia vitendo vya ukatili wa kijinsia vyuoni.
Mkurugenzi Mtendaji shirika la kutetea haki za wanawake na wasichana la KIVULINI, Yassin Ally akiwasilisha mada kuhusu mbinu za kuwasaidia wanafunzi kujitambua, kujiepusha na vitendo vya ukatili wa kijinsia na kuzingatia masomo.
Mdahalo huu kuhusu miaka 40 ya Chuo cha Maendeleo ya Jamii Ufundi (CDTTI) Misungwi mkoani Mwanza unarushwa Mubashara YouTube kupitia BMG TV.

No comments:

Powered by Blogger.