LIVE STREAM ADS

Header Ads

Shirika la Farijika lakabidhi sare za Shule kwa watoto wenye uhitaji jijini Mwanza

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Mkurugenzi wa Shirika la Kutetea Watoto la Farijika (Farijika Community Development and Rights) la jijini Mwanza, Aisha Mtumwa (kulia) akikabidhi sare za shule kwa mwanafunzi wenye uhitaji kwa ajili ya mwaka wa masomo 2023.
Mkurugenzi wa Shirika la Farijika la jijini Mwanza, Aisha Mtumwa (kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi baada ya kupokea sare za shule.
Mkurugenzi wa Shirika la Farijika, Aisha Mtumwa akizungumza wakati wa hafla fupi ya kukabidhi sare za shule kwa wanafunzi wenye uhitaji.
Wazazi,walezi na watoto walioshiriki zoezi la kupokea mahitaji ya shule kutoka shirika la Farijika lenye makazi yake jijini Mwanza.
***

Na Hellen Mtereko, Mwanza
Jamii imehimizwa kuwasaidia watoto wenye uhitaji wakiwemo yatima na wanaoishi kwenye mazingira magumu ili kuhakikisha wanapata huduma muhimu ikiwemo elimu, maladhi, chakula na mavazi hatua itakayowasaidia kutimiza ndoto zao maishani.

Rai hiyo ilitolewa Jumatatu Januari 09, 2023 na Mkurugenzi wa Shirika la kutetea haki za watoto la Farijika (Community Development and Rights) la jijini Mwanza, Aisha Mtumwa wakati akikabidhi sare za shule kwa watoto 70 wenye uhitaji. 

Aisha alisema jamii inapaswa kutambua watoto hao wanastahili kupata haki za msingi kama ilivyo kwa watoto wengine huku akiwahimiza wazazi na walezi kuhakikisha wanafuatilia mwenendo wa watoto wao kwa kuhakikisha wanakwenda shule na kukagua masomo yao wanaporejea nyumbani.

"Pamoja na ubize mlionao wa kutafuta kipatao, inatakiwa mtenge muda wa kufuatilia maendeleo ya watoto wenu kwa kuhakikisha wanafika shule na pia kuwakagua daftari zao ili kubaini ikiwa wanafuatilia masomo yao" alisema Mtumwa.

Aidha Mtumwa aliwaonya baadhi ya walezi ambao wana tabia ya kuwazuia watoto kwenda shule ili wawafanyie kazi za nyumbani na kuwataka kuacha tabia hiyo kwani inawanyika watoto haki yao ya msingi ya kupata elimu.

Nao baadhi ya wazazi na walezi wa watoto waliopokea sare za shule walitoa shukrani kwa Shirika la Farijika kwa namna linavyowasaidia mahitaji mbalimbali ya shule pamoja na chakula.

"Pamoja na Serikali kutoa elimu bila malipo akini bado tunapambana na changamoto ya ukosefu wa fedha za kuwanunulia sare za shule watoto wetu kutokana na ugumu wa maisha tulionao hivyo tunalishukuru sana Shirika hili kwani limekuwa msaada mkubwa kwetu" walieleza.

Itakumbukwa Disemba 18, 2022 shirika la Farijika liliandaa chakula cha mchana kwa watoto yatima na wenye uhitaji jijini Mwanza ambapo wadau walichangia mahitaji mbalimbali ikiwemo sare za shule zilizokabidhiwa Januari 09, 2022.

No comments:

Powered by Blogger.