LIVE STREAM ADS

Header Ads

Waziri Biteko awawashia moto wafanyabiashara wa Kemikali

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Waziri wa Madini, Dkt. Doto Biteko amekasirishwa na hatua ya baadhi ya waagizaji na wasambazaji wa kemikali ya kuchenjulia dhahabu aina ya ‘Sodium Cyanide’ kupandisha kiholela bei ya kemikali hiyo.

Akizungumza katika kikao cha pili cha waagizaji na wasambazaji wa kemikali hiyo kilichofanyika Januari 07, 2022 jijini Mwanza, Dkt. Biteko amesema baadhi ya wafanyabiashara hao wamekuwa wakiuza dumu la kemikali ya ‘Sodium Cyanide’ kati ya shilingi laki nane hadi milioni moja wakati bei elekezi ni shilingi laki sita.

Dkt. Biteko ameongeza kuwa baadhi yao pia wamekuwa wakitoa risiti yenye bei tofauti na mauzo halisi hatua ambayo ni kukwepa kodi na kuwadhurumu wachimbaji wadogo wa madini na hivyo kuagiza hatua kali kuchukuliwa kwa wafanyabiashara watatu waliobainika kujihusisha na mchezo huo.

Awali Rais wa Chama cha Wachimbaji Wadogo wa Madini nchini (FEMATA), John Bina ameshauri Serikali kupitia Shirika la Taifa la Madini (STAMICO) kuanza kuuza kemikali ya ‘Sodium Cyanide’ ambayo ni mbadala wa kemikali ya zebaki ili kuwe na mbadala inapotokea mtikisiko kutoka kwa wafanyabiashara binafsi.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mkurugenzi wa Udhibiti Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Daniel Ndiyo akizungumza kwa niaba ya Mkemia Mkuu wa Serikali na kuahidi kufanyia kazi maelekezo yaliyotolewa na Waziri wa Madini, Dkt. Doto Biteko katika kusimamia biashara ya kemikali ya Sodium Cyanide.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.