LIVE STREAM ADS

Header Ads

Jumuiya ya Wazazi Nyamagana yaadhimisha miaka 46 ya CCM

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Butimba Faustine Ntonja (wapili kulia) akizungumzia umuhimu wa kupanda miti wakwanza kulia ni Mwenyekiti Jumuiya ya wazazi Shabani Mselema watatu ni Meneja Wakala wa huduma za Misitu Wilaya ya Nyamagana Emmanuel Mgimwa.
Meneja Wakala wa Huduma za Misitu Wilaya ya Nyamagana Emmanuel Mgimwa (wapili kushoto) akitoa elimu ya umuhimu wa kupanda miti kweye zoezi la upandaji wa miti katika Hospital ya Wilaya ya Nyamagana.
Balozi wa Mazingira kutoka ofisi ya Makamu wa Rais Mrisho Mabanzo (katikati) akiwa na viongozi wa kata ya Butimba baada ya zoezi la upandaji wa miti katika Hospital ya Wilaya ya Nyamagana.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Butimba Faustine Ntonja (alienyoosha mkono) akiwaelekeza viongozi eneo waliloliandaa kwaajili ya kupanda miti.
Mjumbe wa Baraza Taifa Amini Velji akizungumza na wajumbe wa jumuiya ya wazazi Kata ya Butimba baada ya zoezi la kupanda miti katika Hospital ya Wilaya Nyamagana.
Mjumbe kamati ya utekelezaji balaza Mkoa Wazazi Kambarage Patrick akizungumza na wajumbe wa Jumuiya ya wazazi Kata ya Butimba.
Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi CCM Kata ya Butimba wakipanda miti kwenye Hospital ya Wilaya ya Nyamagana.
Zoezi la upandaji wa miti likiendelea.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Nyamagana Peter Bega akichangia damu.
Katibu wa wazazi Wilaya ya Nyamagana Mariam Msangi akiwa kwenye vipimo vya awali kwaajili ya kuchangia damu.
***

Na Hellen Mtereko, Mwanza
Jumuiya ya wazazi Wilaya ya Nyamagana Mkoani Mwanza imeadhimisha kumbukizi ya miaka 46 ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)kwa kupanda miti katika maeneo mbalimbali ikiwemo Hospital ya Wilaya ya Nyamagana pamoja na kuchangia damu ili kuokoa maisha ya wenye uhitaji.

Jumuiya hiyo imefanya shughuli hizo za kijamii leo Januari 27,2023 katika Kata ya Igoma na Butimba.

Katibu wa wazazi Wilaya ya Nyamagana Mariam Msangi, amesema walizindua Maadhimisho hayo Januari 25,2023 kwenye Kata zote za Wilaya hiyo huku wakifanya shughuli mbalimbali ikiwemo kuingiza wanachama wapya,kupanda miti pamoja na kuchangia damu.

"Jumuiya ya wazazi tumehitimisha sherehe za miaka 46 leo katika Kata ya Igoma,tumefanikiwa kuingiza wanachama wapya 920,tumepanda miti 2300 katika kata zote za Wilaya ya Nyamagana, tumeingiza wanachama wapya 16 kutoka vyama vya upinzani pamoja na kuchangia damu hivyo", amesema Msangi.

Kwaupande wake Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Nyamagana Peter Bega, amesema Feburuari 5,2023 Chama hicho kinatimiza miaka 46 na ndio maana leo Jumuiya ya wazazi wamefanya shughuli mbalimbali za kijamii kwaajili ya kutimiza ilani.

Bega amesema wamekuwa wakipanda miti katika taasisi mbalimbali ili kuifanya Mwanza kuwa ya kijani huku akiwaomba wananchi waendelee kutunza miti hatua itakayosaidia kuachana na tabia ya ukataji wa miti kiholela.

awali akizungumza kwenye zoezi la upandaji wa miti katika Hospital ya Wilaya ya Nyamagana mjumbe wa Baraza Taifa Amini Velji, amesema miti inaumuhimu mkubwa sana katika Taifa hivyo jamii inapaswa kuwa na utaratibu wa kutunza miti kuanzia kweye ngazi ya familia na jamii kwa ujumla.

Katika hatua nyingine Jumuiya hiyo imechangia damu kwa lengo la kuwasaidia wahitaji huku ikiiomba jamii kujitoa kwaajili ya kuchangia kwani mahitaji ni makubwa.

Mussa Ngoro ni Diwani wa Kata ya Igoma amesema, hakuna kiwanda kinachozalisha damu hivyo kila mtu anawajibu wa kuchangia damu katika kuokoa maisha ya wahitaji damu.

" Wanaochangia damu nao ni wahitaji damu kwasababu hakuna mtu anayejua atapata mahitaji ya damu wakati gani", amesema Ngoro.

No comments:

Powered by Blogger.