Wachimbaji madini 159 nchini, wapoteza maisha migodini, 59 wajeruhiwa
Mkurugenzi wa Huduma za Sheria Tume ya Madini Dk. Anold Gasase akizungumza wakati akifungua mafunzo yanayowahusisha wachimbaji wadogo wa kanda ya kati yanayofanyika mkoani hapa. Mafunzo hayo yaliyoandaliwa na Tume ya Madini yameanza Januari 26, 2023 na yatafikia tamati Januari 27, 2023.
Na Dotto Mwaibale, Singida
WACHIMBAJI wadogo wa madini 139 nchini wamepoteza
maisha katika maeneo ya migodi huku 59 wakijeruhiwa katika kipindi cha mwaka
1918 hadi 1919 na 2019-2020.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Huduma za Sheria Tume ya
Madini Dk. Anold Gasase wakati akifungua mafunzo yanayowahusisha wachimbaji
wadogo wa kanda ya kati yenye lengo la kuelimisha, kukumbushana masuala ya
usalama, baruti, uhifadhi wa mazingira katika maeneo ya uchimbaji mdogo yanayofanyika
mkoani hapa.
Alisema
mafunzo hayo ambayo yanatolewa na wataalam mbalimbali kutoka Tume ya Madini
yana lenga kuhakikisha shughuli za uchimbaji wa madini na uchanjuaji wa madini
zinafanyika katika mazingira yenye kuzingatia usalama, afya na taratibu na
miongozo mbalimbali iliyotolewa.
“Shughuli
za uchimbaji na uhanjuaji wa madini zinamanufaa makubwa kwa wachimbaji na taifa
kwa ujumla kupitia fursa za ajira, biashara pamoja na kodi mbalimbali” alisema
Gasase.
Alisema
pamoja na manufaa hayo shughuli hizo zimekuwa zikikutana na matukio ya ajali,
madhara ya kiafya, uhalibifu wa mazingira kwenye baadhi ya machimbo na kusa na
kusababisha vifo na majeruhi hali ambayo sio afya katika sekta ya madini.
Alisema uchunguzi uliofanyika unaonesha kwamba ajali hizo zinasababishwa na kuanguka kwa mashmo na kuwafukia wachimbaji na kukosekana kwa hewa ndani ya mashimo ya uchimbaji.
Aidha
Gasase alisema tafiti zinaonesha ajali nyingi, athari za kiafya na uhalibifu wa
mazingira migodini zinasababishwa na uzingatiaji mdogo na elimu ya masuala ya
usalama, afya na utunzaji wa mazingira miongoni mwa wachimbaji.
Alisema
shughuli za uchimbaji zinahusisha utunzaji na usafirishaji wa baruti ambazo
zinaambatana na usalama, kiafya na
uhalibifu wa mazingira ambapo sheria ya baruti ya mwaka 1963 na kanuni zake za
mwaka 1964 zisipozingatiwa na wasambaji na watumiaji wa baruti.
Dk.Gasase
alitumia nafasi hiyo kuwaomba washiriki wa mafunzo hayo kujifunza kwamakini na
kuuliza maswali ili waweze kujua mambo mbalimbali yanayohusu sheria za
uchimbaji na mengineyo.
Mwenyekiti
wa wachimbaji wadogo Mkoa wa Singida Robert Malando alisema changamoto kubwa
waliyonayo ni kukatika mara kwa mara kwa umeme ambapo waliomba Tume ya Madini
na Serikali iwasaidie.
Baadhi ya wachimbaji wa madini waliohudhuria mafunzo hayo wameipongeza Tume ya madini kwa kuwapelekea mafunzo hayo ambayo yamewaongezea uelewa na ujasiri na kuwa hawataogopa kwenda kulipa kodi tofauti na hap awali alisema Magdalena Lucas ambaye ni mchimbaji wa madini kutoka mgodi wa Mpipiti.
Mada zilizotolewa kwenye mafunzo hayo ni Sheria ya madini, Taratibu za upatikanaji wa leseni kwa wachimbaji wa madini, Taratibu za usimamizi wa mgodi, Usalama na afya migodini na Usimamizi wa baruti.
No comments: