LIVE STREAM ADS

Header Ads

Watoa huduma za Bima watakiwa kutumia lugha ya Kiswahili

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Makampuni ya Bima na Watoa huduma za Bima nchini wametakiwa kutoa hati ya malipo kwa lugha ya Kiswahili ili kuondoa migogoro inayojitokeza kati ya waathirika na watoa huduma za Bima wakati wa malipo.

Kauli hiyo imetolewa na kamishina wa Bima Dkt Baghayo Saqware wakati wa kikao cha kupokea na kusikiliza mamalamiko ya watumia huduma za Bima kutoka kanda ya ziwa.

Dkt Saqware amesema wananchi wengi wamepoteza haki zao kwa kushindwa kuelewa vizuri lugha inayotumika katika hati ya malipo na wengi wao kupata uelewa baada ya kulipwa malipo pungufu.

“sisi mamlaka huku nyaraka zetu zote kwa hivi sasa zinasomeka kwa lugha ya Kiswahili na Kingereza ni matarajio yangu kabla mwaka wa 2024 haujaisha kila kitu kitakuwa kikiandikwa kwa Kiswahili”.alisema Dkt Saqwaya.

Kamishina amesema lengo la Mamlaka ni kuhakikisha nyaraka zote zinaandaliwa kwa lugha ya Kiswahili na kuwataka wadau wa Bima kuanza na Hati ya Malipo ambayo ni muhimu kwa hivi sasa kwa kuwa inawagusa wananchi wengi hasa wahanga wa ajali.

Awali akitoa mamalamiko yake ya kucheleweshewa fidia yake na kampuni ya G.A INSURANCE (T) LTD Jackline Patrick Katona mkazi wa Nyakato jijini Mwanza amesema baada ya kuhangaikia fidia yake kwa muda mrefu alipewa nyaraka za malipo azisome lakini hakuzielewa kwa kuwa ziliandikwa kwa lugha ya kingereza.

“Kamishina mimi ndio namsikia meneja hapa akisema malipo yangu tayari lakini mimi sikujua maana walinipa makaratasi mengi niyasome na yameandikwa kingereza hivyo sikuelewa chochote kwa kweli”.alisema Jackline.
Kwa upande wake mshiriki kutoka kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Mwanza Sajenti Jeremiah Makeremu ameiomba mamlaka ya Bima kuangalia tatizo la kimtandao ambalo wamekuwa wakikutananalo wakati wa kuhakiki Bima za magari.
Akijibu tatizo hilo mtaalamu wa IT kutoka mamlaka ya Bima Seif Bakari amesema watawasiliana na jeshi la Polisi kuona na namna gani ya kulitatua tatizo hilo na kulipa wepesi jeshi la polisi katika utendaji wake wa kazi wa kila siku.

Akihitimisha kikao hicho cha kupokea na kusikiliza Malalamiko ya wadau wa Bima, Kamishina Dkt Saqware amewataka wananchi wote kuitumia mamlaka ya Bima pale wanapohisi kukosa haki zao kutoka kwa watoa huduma ili kutafuta njia kutatua matatizo waliyonayo.
Wadau wa bima.
Na Tonny Alphonce, Mwanza

No comments:

Powered by Blogger.