LIVE STREAM ADS

Header Ads

Mbunge Mabula akabidhi Vyeti vya Pongezi kwa Waalimu Butimba jijini Mwanza

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Mbunge wa Jimbo la Nyamagana, Stanslaus Mabula (kulia) akimkabidhi cheti vya pongezi mmoja wa waalimu wa Shule za Msingi Kata ya Butimba ikiwa ni sehemu ya kutambua jitihada zao zilizosaidia kuongeza kuongeza ufaulu katika matokeo ya darasa la saba ambapo kati ya Shule nane za Kata hiyo, Shule sita wanafunzi wake walipata ufaulu wa alama A na B tu huku Shule mbili zikiwa na ufaulu wa alama A, B na C.
***

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mbunge wa Jimbo la Nyamagana (CCM), Stanslaus Mabula amekabidhi vyeti vya pongezi kwa waalimu waliofanya vizuri katika masomo yao na kusaidia kuinua kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi wa darasa la saba waliohitimu mwaka jana.

Mabula alikabidhi vyeti hivyo katika hafla ya kuwapongeza waalimu wa Shule za Msingi Kata ya Butimba jijini Mwanza iliyofanyika Februari 21, 2023 huku akitumia fursa hiyo kuwahimiza waalimu kufanya kazi kwa bidii na uadilifu wakati Serikali ikiendelea kuboresha maslahi yao.

Aidha aliwapongeza waalimu hao kwa jitihada zao zilizosaidia wanafunzi wa darasa la saba kufaulu kwa alama A na B katika shule sita za Kata ya Butimba huku Shule mbili tu zikiwa na ufaulu wa alama A, B na C ambazo pia waalimu wake wameahidi kuondoa ufaulu wa alama C katika mtihani ujao.

Mabula pia alimpongeza Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa dhamira yake njema ya kuendelea kuboresha miundombinu ya elimu ikiwemo ujenzi wa vyumba vya madarasa pamoja na maslahi ya waalimu ili kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao kwa ufanisi.

Pia Mabula aliahidi kusaidia upatikanaji wa mashine ya kudurufu karatasi (Photocopy Machine) pamoja na komputa kwa ajili ya Ofisi ya Afisa Elimu Kata ya Butimba huku akitoa mchango wa shilingi milioni moja kwa ajili ya manunuzi ya karatasi (ream paper).

Naye Afisa Elimu Kata ya Butimba, Mwl. Cecilia Tegile alisema Serikali imeendelea kuwa sikivu kwa kutatua changamoto za waalimu ikiwemo upandishaji madaraja na kulipa madeni yao huku akitoa shukurani kwa uamuzi wake wa kugawa vishikwambi kwa waalimu wote nchini.
Mbunge wa Jimbo la Nyamagana, Stanslaus Mabula akikabidhi vyeti vya pongezi kwa waalimu wa Shule za Msingi Kata ya Butimba waliofanya vizuri na kuongeza ufaulu katika matokeo ya darasa la saba.
Mbunge wa Jimbo la Nyamagana, Stanslaus Mabula akikabidhi vyeti vya pongezi kwa waalimu wa Shule za Msingi Kata ya Butimba waliofanya vizuri na kuongeza ufaulu katika matokeo ya darasa la saba.
Mbunge wa Jimbo la Nyamagana, Stanslaus Mabula akikabidhi vyeti vya pongezi kwa waalimu wa Shule za Msingi Kata ya Butimba waliofanya vizuri na kuongeza ufaulu katika matokeo ya darasa la saba.
Mgeni rasmi, Mbunge wa Jimbo la Nyamagana (CCM), Stanslaus Mabula akizungumza na waalimu wa Shule za Msingi Kata ya Butimba kwenye hafla ya kuwapongeza baada ya kufanya vizuri katika matokeo ya darasa la saba.
Afisa Elimu Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Mwl. Mussa Lambwe akizungumza kwenye hafla hiyo ya kuwapongeza waalimu Kata ya Butimba kutokana na ufaulu mzuri kwenye matokeo ya darasa la saba.
Afisa Elimu Kata ya Butimba jijini Mwanza, Mwl. Cecilia Tegile akizungumza wakati wa hafla ya kuwapongeza waalimu wa Kata hiyo kutokana na jitihada zao zilizosaidia wanafunzi kupata ufaulu mzuri katika mtihani wa darasa la saba.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Nyamagana, Kalebe Luteli akitoa salamu kwa niaba ya Mwenyekiti wa CCM Wilaya Nyamagana.
Mwenyekiti wa CCM Kata ya Butimba jijini Mwanza, Faustine Ntoja akitoa salamu wakati wa hafla hiyo.
Katibu Mwenezi wa CCM Kata ya Butimba, Jumanne Mansoor akitoa salamu zake wakati wa hafla hiyo.
Mbunge wa Jimbo la Nyamagana, Stanslaus Mabula akiongoza zoezi la kukata na kula keki.
Waalimu Kata ya Butimba wakicheza muziki pamoja na mgeni rasmi Mbunge wa Jimbo la Nyamagana, Stanslaus Mabula wakati wa hafla ya kuwapongeza kwa kufanya vizuri kwenye matokeo ya darasa la saba.

No comments:

Powered by Blogger.