Wanawake Hospitali ya Bugando waadhimisha 'Siku ya Wanawake Duniani'
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Wanawake watumishi katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Bugando jijini Mwanza wameadhimisha siku ya wanawake duniani ambayo kilele chake ni Machi 08, 2023, huku wakitakiwa kusimama imara na kutojiona wanyonge katika kutimiza malengo yao.
Maadhimisho hayo yamefanyika Machi 06, 2023 hospitalini hapo huku mgeni rasmi akiwa ni Linarda Muindi (Mrs. Zongii) ambaye ni miongoni mwa wanawake wafanyabiashara na wawekezaji wakubwa jijini Mwanza.
Katika hafla hiyo, Mrs. Zongii aliwahimiza wanawake kuwa imara na kuhakikisha hawavumilii vitendo vya ukatili wa kijinsia hususani katika ndoa. Aliwashauri kutathimini aina ya wenza wanaokuwa nao maishani na kuhakikisha ni aina ya wenza ambao wanaweza kushirikiana pamoja na kufikia malengo yao.
Naye Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu kutoka Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Bugando jijini Mwanza, Jacqueline Kidunda alisema hapo awali wanawake/ watoto wa kike walikumbana na changamoto za kiusawa ikiwemo kutopata haki sawa kielimu na watoto wa kiume lakini dhana hiyo sasa haipo hivyo hakuna vikwazo vya kuwafanya wasitimize ndoto zao.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa wanawake katika Hospitali ya Bugando, Eunice Kitula aliwasihi wanawake kuwa wabunifu na kutumia fursa zinazowazunguka ili kufikia mafanikio yao kuendana na kuli mbiu ya siku ya wanawake 2023 isemayo "Ubunifu na Mabadiliko ya Teknolojia: Chachu katika Kuleta Usawa wa Kijinsia".
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu kutoka Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Bugando jijini Mwanza, Jacqueline Kidunda akizungumza kwenye hafla ya wanawake watumishi wa Hospitali hiyo iliyofanyika Jumatatu Machi 06, 2023 ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani aambayo kilele chake ni Jumatano Machi 08, 2023.
Mwenyekiti wa Wanawake Hospitali ya Bugando (BMC), Eunice Kitula akizungumza wakati wa hafla ya Siku ya Wanawake Duniani 2023 iliyoadhimishwa hospitalini hapo Machi 06, 2023.
Mgeni rasmi, Linarda Muindi (Mrs. Zongii) akizungumza na wanawake watumishi wa hospitali ya Rufaa Kanda ya Bugando jijini Mwanza ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani 2023..
Mkurugenzi wa Huduma za Uuuguzi BMC, Sr. Salome Marandu akitoa salamu zake wakati wa hafla hiyo.
Mkurugenzi wa Huduma za Upasuaji BMC, Dkt. Sr. Alicia Massenga akizungumza wakati wa hafla hiyo.
Wanawake watumishi wa BMC na wageni waalikwa wakipata shampeini.
Wanawake watumishi wa BMC wakigonga chiazi meza kuu na mgeni rasmi, Linarda Muindi- Mrs. Zongii (wa pili kushoto).
Wanawake watumishi wa BMC wakigonga chiazi meza kuu na mgeni rasmi, Linarda Muindi- Mrs. Zongii (wa pili kushoto).
Mwenyekiti wa Wanawake Hospitali ya Bugando (BMC), Eunice Kitula (kushoto) akimlisha keki mgeni rasmi, Linarda Muindi- Mrs. Zongii (wa pili kulia).
Mgeni rasmi, Linarda Muindi- Mrs. Zongii (wa pili kulia) akimlisha keki Mwenyekiti wa Wanawake Hospitali ya Bugando (BMC), Eunice Kitula (wa pili kushoto).
Mgeni rasmi, Linarda Muindi- Mrs. Zongii ( kulia) akiwalisha keki watumishi wanawake wa BMC wakati wa hafla ya Siku ya Wanawake 2023.
Watumishi wanawake wa Hosipitali ya Rufaa Kanda ya Bugando jijini Mwanza wakipata shampeini.
Mwenyekiti wa Wanawake Hospitali ya Bugando (BMC), Eunice Kitula (kushoto) akikabidhi tuzo kwa mgeni rasmi, Linarda Muindi- Mrs. Zongii (kulia) ikiwa ni sehemu ya kutambua mchango wake katika jamii akiwa miongoni mwa wanawake wanaowasaidia wanawake wengine ili kupiga hatua kimaendeleo.
Wanawake watumishi wa BMC wakiwa kwenye hafla ya Siku ya Wanawake Duniani iliyofanyika hospitalini hapo Machi 06, 2023 kabla ya kilele cha maadhimisho yatakayofanyika kimkoa wilayani Kwimba Machi 08, 2023.
Kauli mbiu siku ya wanawake duniani 2023 ni "Ubunifu na Mabadiliko ya Teknolojia: Chachu katika Kuleta Usawa wa Kijinsia".
No comments: