LIVE STREAM ADS

Header Ads

Wanawake TANESCO Mwanza wapanda miti kuelekea kilele cha 'Siku ya Wanawake Duniani'

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Katika kuelekea kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Machi 08, 2023, wanawake watumishi wa shirika la umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa Mwanza, wamepanda miti katika Zahanati ya Mahina jijini Mwanza ikiwa ni sehemu ya hamasa ya upandaji miti nchini ili kuimarisha uoto wa asili utakaosaidia upatikanaji wa mvua na hivyo kuimarisha vyanzo vya maji kwa ajili ya kuzalisha umeme.

Zoezi hilo la upandaji miti limefanyika Jumanne Machi 07, 2023 likiongozwa na Mkuu wa Wilaya Nyamagana, Amina Makilagi ambaye amewapongeza wanawake watumishi wa TANESCO kwa wazo lao la kupanda miti na kuwasihi wadau wengine kuiga mfano huo.

Makilagi amesema shirika la TANESCO limekuwa likitegemea kwa kiasi kikubwa miti kwa ajili ya kusambaza huduma ya umeme hivyo uamuzi wa kuhamasisha upandaji wa miti utasaidia kukabiliana na athari za kimazingira na hivyo kuagiza zoezi hilo liwe endelevu.

Ameagiza TANESCO Mkoa Mwanza kushirikiana na Ofisi ya Afisa Mazingira Halmashauri ya Jiji la Mwanza pamoja na Wakala wa Huduma za Misiti (TFS) kutafuta maeneo zaidi na kuhamasisha upandaji wa miti ili kufikia lengo la Mkoa Mwanza la kupanda miche milioni 1.5 huku pia wakihakikisha miche hiyo inatunzwa na kukua vyema.

Meneja wa TANESCO Mkoa Mwanza, Mhandisi Said Msemo amekiri kupokea agizo hilo na kuahidi kulifanyia kazi akisema TANESCO shirika la TANESCO lazima liwe mstari wa mbele kuhamasisha upandaji miti kwani limekuwa likitegemea miti kwa ajili ya nguzo za umeme.

Naye Afisa Masoko TANESCO Mkoa Mwanza, Joyce Makori amesema upandaji miti kwa wingi unasaidia mvua kunyesha na hivyo kusaidia uzalishaji wa umeme wa uhakika ndiyo maana TANESCO imekuja na hamasa ya kupanda miti nchini kupitia kaulimbiu isemayo "panda miti, mvua ndii, umeme ndindii"

Kwa upande wake Mhifadhi Misitu kutoka TFS Wilaya ya Nyamagana, Emmanuel Mgimwa amesema taasisi hiyo imetoa bure miche 120 ya aina mbalimbali ikiwemo matunda na kimvuli kwa ajili ya kuunga mkono jitihada za kupanda miti za wanawake watumishi wa TANESCO na kwamba taasisi hiyo itaendelea kushirikiana na shirika hilo pamoja na wadau wengine kuhakikisha zoezi la upandaji miti linakuwa endelevu katika jamii ili kutunza mazingira na kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mkuu wa Wilaya Nyamagana mkoani Mwanza, Amina Makilagi akizungumza wakati wa zoezi la kupanda miti katika Zahanati ya Mahina jijini Mwanza ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yaliyofanywa na wanawake watumishi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa Mwanza, Machi 07, 2023.
Meneja wa TANESCO Mkoa Mwanza, Mhandisi Said Msemo (kulia) akizungumza wakati wa zoezi la kupanda miti lililoandaliwa na wanawake watumishi wa shirika hilo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani 2023.
Afisa Masoko TANESCO Mkoa Mwanza, Prisca Kayagi (kushoto) akieleza lengo la kupanda miti ni pamoja na kusaidia upatikanaji wa mvua utakaowezesha kupata maji ya uhakika kwa ajili ya uendeshaji wa mitambo inayozalisha umeme nchini.
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Amina Makilagi akiongoza zoezi la upandaji miti katika Zahanati ya Mahina.
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Amina Makilagi akipanda mche katika Zahanati ya Mahina ikiwa ni shamra shamra za wanawake watumishi wa TANESCO Mkoa Mwanza kuelekea kilele cha Siku ya Wanawake Duniani, Machi 08,2023.
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Amina Makilagi akipanda mche katika Zahanati ya Mahina ikiwa ni shamra shamra za wanawake watumishi wa TANESCO Mkoa Mwanza kuelekea kilele cha Siku ya Wanawake Duniani, Machi 08,2023.
Meneja wa TANESCO Mkoa Mwanza, Mhandisi Said Msemo akipanda mche katika Zahanati ya Mahina.
Meneja wa TANESCO Mkoa Mwanza, Mhandisi Said Msemo akipanda mche katika Zahanati ya Mahina.
Diwani Kata ya Mahina jijini Mwanza, Alphonce Francis (kulia) akipanda mche katika Zahanati ya Mahina kuunga mkono jitihada za wanawake watumishi wa TANESCO Mkoa Mwanza.
Mwenyekiti wa CCM Kata ya Mahina, Halima Luhunga akipanda mche katika Zahanati ya Mahina wakati wa zoezi la kupanda miche lililoandaliwa na wanawake watumishi wa TANESCO Mkoa Mwanza.
Zoezi la kupanda miche ya aina mbalimbali ikiwemo ya matunda na kimvuli likiendelea katika Zahanati ya Mahina ikiwa ni ushirikiano wa pamoja baina ya wanawake watumishi wa TANESCO Mkoa Mwanza na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) ambao wametoa bure miche 120.
Zoezi la kupanda miche ya aina mbalimbali ikiwemo ya matunda na kimvuli likiendelea katika Zahanati ya Mahina ikiwa ni ushirikiano wa pamoja baina ya wanawake watumishi wa TANESCO Mkoa Mwanza na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) ambao wametoa bure miche 120.
Wanawake watumishi wa TANESCO Mkoa Mwanza wakiwa kwenye zoezi la kupanda miti katika Zahanati ya Mahina ikiwa ni shamra shamra za kuelekea kwenye kilele cha maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yatakayofanyika Machi 08, 2023.
Sehemu ya mwonekano wa Zahanati ya Mahina jijini Mwanza.

No comments:

Powered by Blogger.