LIVE STREAM ADS

Header Ads

MWANZA: Mawakala wa CRDB kuibuka na zawadi nono wakisherehekea miaka 10

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Katika kuadhimisha miaka 10 tangu kuanzishwa huduma ya CRDB Wakala, benki ya CRDB imetenga zawadi mbalimbali ikiwemo kamisheni za fedha, bodaboda, bajaji na gari kwa ajili ya kuwazawadia mawakala wake watakaowahudumia wateja wengi zaidi kwa kipindi cha miezi minne mfululizo ijayo.

Meneja wa benki ya CRDB tawi la Mwanza, Jeremiah Msemo ameyasema hayo Aprili 25, 2023 wakati akizungumza kwenye semina ya mawakala wa benki hiyo mkoani Mwanza, iliyolenga kuwajengea uwezo ili kuendelea kutoa huduma bora zaidi kwa wateja.

Amesema huduma ya CRDB Wakala iliyoanzishwa mwaka 2013 imesaidia kuondoa kero mbalimbali ikiwemo foleni katika matawi mbalimbali ya benki hiyo huku ikitoa ajira kwa mawakala zaidi ya elfu 25 ambao nao wameajiri vijana mbalimbali ambao wanajipatia kipato.

Msemo ametumia fursa hiyo kuwapongeza mawakala wote wa CRDB kwa kutoa huduma karibu na wananchi na kubainisha kuwa kutokana na umuhimu wao, benki ya CRDB imekuja na kampeni ya kuwazawadia mawakala watakaotoa huduma kwa wateja wengi zaidi akisema zawadi hizo ni fedha/ kamisheni, bodaboja 40, bajaji tano na gari moja aina ya Alphard.

Naye Meneja Mawakala CRDB, Goodluck Ruhago amesema huduma ya CRDB Mawakala imeboreshwa zaidi ambapo hivi sasa huduma zinazopatikana katika matawi ya benki hiyo pia zinapatikana kwa mawakala ikiwemo kufungua akaunti, kuweka na kutoa pesa pamoja na kulipia bili na kodi mbalimbali na hivyo kupunguza foleni kwa wateja wanaohitaji huduma za kibenki.

Kwa upande wake Meneja Uendeshaji Bima kutoka benki ya CRDB, Tumaini Frank amesema hivi sasa huduma ya kulipia bima mbalimbali ikiwemo bima za vyombo vya moto inapatikana kwa mawakala wa benki hiyo na kuondoa usumbufu kwa wateja.

Akifungua semina hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza Hassan Masala ameipongeza benki ya CRDB kwa maboresho makubwa ya huduma na mifumo iliyoyafanya ikiwemo kuwezesha wateja kufungua akaunti mbalimbali ikiwemo Al-Barak inayofuata misingi ya dini ya kiislamu pamoja na huduma ya bima kwa mawakala ambayo itasaidia lengo la Serikali la kufikisha huduma za bima kwa wananchi kwa kiwango cha asilimia 60.

Nao baadhi ya mawaka wa benki ya CRDB walioshiriki semina hiyo akiwemo Rose Mnangu wamesema zawadi zilizotangazwa kutolewa kwa mawakala watakaowahudumia wateja wengi zaidi zinatoa hamasa kwao kuendelea kutoa huduma bora kwa wateja huku wakiishukuru benki hiyo kwa kutambua huduma wanayoitoa.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mkuu wa Wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza, Hassan Masala (kushoto) akizungumza wakati wa ufunguzi wa semina kwa Mawakala wa Benki ya CRDB iliyofanyika Aprili 25, 2023 jijini Mwanza. Kulia ni Meneja wa CRDB Tawi la Mwanza, Jeremiah Msemo na katikati ni Meneja Uendeshaji Bima kutoka CRDB, Tumaini Frank.
Meneja wa CRDB Tawi la Mwanza, Jeremiah Msemo akizungumza wakai wa semina kwa Mawakala wa benki hiyo jijini Mwanza.
Meneja wa CRDB Tawi la Mwanza, Jeremiah Msemo (kulia) akizungumza kwenye semina hiyo iliyoambatana na uzinduzi wa kampeni ya kuwazawadia mawakala watakaohudumia wateja wengi zaidi ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha miaka 10 tangu kuanzishwa huduma ya CRDB Wakala.
Meneja Mawakala Benki ya CRDB, Goodluck Ruhago amesema huduma ya CRDB Wakala ilianzishwa mwaka 2013 ikiwa na mawakala 300 lakini hadi kufikia mwaka huu 2023 ikiwa ni miaka 10, huduma hiyo ina zaidi ya mawaka elfu 25 na hivyo kurahisisha upatikanaji wa huduma za kibenki karibu na wananchi.
Baadhi ya Mawakala wa Benki ya CRDB jijini Mwanza wakifuatilia semina ya kuwajengea uwezo kutoa huduma bora kwa wananchi hatua itakayowawezesha kujishindia zawadi mbalimbali ikiwemo kamisheni, bodaboda, bajaji na gari.
Katika kuboresha huduma za Mawakala wa CRDB, sasa watakuwa na uwezo wa kusajili na kufanya malipo ya bima mbalimbali ikiwemo ya vyombo vya moto pamoja na wateja kufungua akaunti mbalimbali ikiwemo Al- Barak inayofuata misingi ya dini ya kiislamu.
Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Hassan Masala (kulia), Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Mwanza Jeremiah Msemo (katikati) na Meneja Uendeshaji Bima kutoka Benki ya CRDB Makao Makuu Tumaini Frank (kushoto) wakiwa kwenye semina ya kuwajengea uwezo Mawakala wa CRDB jijini Mwanza (hawako pichani).
Baadhi ya viongozi wa benki ya CRDB wakiwa kwenye semina hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Ilemela, Hassan Masala (wa pili kulia) akikabidhi cheti cha utambuzi kwa mmoja wa mawakala wa benki ya CRDB (kushoto) ambaye alianza kutoa huduma hiyo miaka 10 iliyopita.
Mkuu wa Wilaya ya Ilemela, Hassan Masala (kulia) akikabidhi cheti cha utambuzi kwa mmoja wa mawakala wa benki ya CRDB (kushoto) ambaye alianza kutoa huduma hiyo miaka 10 iliyopita.
Mkuu wa Wilaya ya Ilemela, Hassan Masala (kulia) akikabidhi cheti cha utambuzi kwa mmoja wa mawakala wa benki ya CRDB (kushoto) ambaye alianza kutoa huduma hiyo miaka 10 iliyopita.
Mkuu wa Wilaya ya Ilemela, Hassan Masala (kulia) akikabidhi cheti cha utambuzi kwa mmoja wa mawakala wa benki ya CRDB (kushoto) ambaye alianza kutoa huduma hiyo miaka 10 iliyopita.
Huduma ya CRDB Wakala ilianzishwa mwaka 2013 ambapo mwaka huu 2023 imetimiza miaka 10 hivyo benki ya CRDB imekuja na kampeni ya "Miaka 10 Pamoja Nawe" ambapo mawakala watakaotoa huduma kwa wateja wengi zaidi watajishindia kamisheni za fedha, bodaboda, bajaji na gari.
Mkuu wa Wilaya ya Ilemela, Hassan Masala (katikati) akikabidhi cheti cha utambuzi kwa mmoja wa mawakala wa benki ya CRDB (kushoto) ambaye alianza kutoa huduma hiyo miaka 10 iliyopita. Kulia ni Meneja wa CRDB tawi la Mwanza, Jeremiah Msemo.
Mkuu wa Wilaya ya Ilemela, Hassan Masala (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na Mawakala wa CRDB jijini Mwanza walioanza kutoa huduma hiyo miaka 10 iliyopita.
Viongozi mbalimbali meza kuu akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Ilemela (wa tatu waliokaa) wakiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya Mawakala wa benki ya CRDB jijini Mwanza.
Viongozi mbalimbali meza kuu akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Ilemela (wa tatu waliokaa) wakiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya Mawakala wa benki ya CRDB jijini Mwanza.
Baadhi ya viongozi wa benki ya CRDB wakijitambulisha kwa mawakala wa benki hiyo jijini Mwanza (hawako pichani) waliohudhuria semina ya kuwajengea uwezo kutambua huduma zinazotolewa na CRDB ili wakasaidie kuongeza wateja na kujishindia zawadi mbalimbali.
Baadhi ya Mawakala wa Benki ya CRDB jijini Mwanza wakiwa kwenye semina ya kuwajengea uwezo ili kuendelea kutoa huduma bora kwa wateja huku wakijishindia zawadi mbalimbali ikiwemo fedha, bodaboda, bajaji na gari ikiwa ni sehemu ya kusherehekea miaka 10 tangu kuanzishwa huduma ya CRDB Mawakala.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.