LIVE STREAM ADS

Header Ads

RC Mwanza aitaka LVRLAC kusimamia ipasavyo rasilimali za Ziwa Victoria

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Adam Malima amezitaka Halmashauri wanachama wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa (LVRLAC) Kanda ya Tanzania kusimamia ipasavyo rasilimali za Ziwa Victoria ili ziendelee kuwa na tija kwa wananchi.

Malima ameyasema hayo Machi 31, 2023 wakati wa mkutano mkuu wa 27 wa jumuiya hiyo uliofanyika jijini Mwanza na kuongeza kuwa madiwani pia wana wajibu mkubwa wa kuhakikisha wanaweka mikakati itakayosaidia ongezeko la rasilimali za Ziwa Victoria ikiwemo samaki na

Mwenyekiti LVRLAC Kanda ya Tanzania, William Gumbo amesema jumuiya hiyo inayoundwa na nchi za Tanzania, Kenya na Uganda ina jumla ya Halmashauri 130 zinazozunguka Ziwa Victoria na imekuwa ikihamasisha utunzaji wa mazingira ya Ziwa hilo kwa manufaa ya wananchi wanaolizunguka.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Adam Malima akizungumza kwenye Mkutano wa LVRLAC.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Adam Malima akizungumza kwenye Mkutano wa LVRLAC.
Mwenyekiti wa LVRLAC, William Gumbo akizungumza kwenye mkutano wa jumuiya hiyo uliofanyika jijini Mwanza.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.