LIVE STREAM ADS

Header Ads

Uchumi wa Tanzania wapaa miaka miwili ya Rais Samia - IMF

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Pato la Taifa lafikia Sh. trilioni 200 kwa mwaka 2023 kutoka Sh. trilioni 163 ya mwaka 2021

Uchumi wa Tanzania sasa ni mkubwa kuliko baadhi ya nchi za Ulaya na ni wa 6 kwa ukubwa kwa nchi zote za Kusini mwa Jangwa la Sahara

IMF yabashiri Pato la Taifa la Tanzania kufikia karibu Sh. trilioni 300 ndani ya miaka mitano ijayo

Na Mwandishi Maalum 
 
Takwimu mpya za Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) zinaonesha kuwa Pato la Taifa la Tanzania kwa bei ya sasa limeongezeka hadi kufikia Dola za Marekani Bilioni 85.42 (Shilingi trilioni 200) kwa mwaka huu wa 2023, ikiwa ni ishara kuwa sera za uchumi za Rais Samia Suluhu Hassan zinaleta mageuzi makubwa nchini.

Ongezeko hilo la Pato la Taifa ni kutoka Dola za Marekani Bilioni 69.9 (Shilingi trilioni 163.5) kwa mwaka 2021, wakati ambapo Rais Samia alipoingia madarakani.

Takwimu hizo za IMF zinaonesha kuwa Pato la Taifa la Tanzania huenda likaongezeka zaidi hadi kufikia Dola za Marekani Bilioni 136.09 (Sh. trilioni 276) ifikapo mwaka 2028.

Tangu alipoingia madarakani Machi 2021, Rais Samia ametekeleza sera rafiki kwa sekta binafsi, ambayo imeongeza kasi ya uwekezaji, biashara na ukuaji wa uchumi nchini.

Kwa mujibu wa takwimu hizo mpya za IMF, Pato la Taifa la Tanzania kwa mwaka 2023 ni kubwa kuliko nchi kadhaa ndogo za Ulaya, ikiwemo Croatia ($78.8 billion), Lithuania ($78.3 billion), Serbia ($73.9 billion) and Slovenia ($68.1 billion).

Kwa upande wa nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara, Tanzania ni nchi ya 6 kwa ukubwa wa Pato la Taifa.

Kwa mujibu wa takwimu za IMF, nchi kumi zinazoongoza kwa ukubwa wa Pato la Taifa Kusini mwa Jangwa la Sahara ni hizi zifuatazo:

1. Nigeria $506.6 billion ๐Ÿ‡ณ๐Ÿ‡ฌ

2. South Africa $399 billion ๐Ÿ‡ฟ๐Ÿ‡ฆ

3. Ethiopia $156 billion ๐Ÿ‡ช๐Ÿ‡น

4. Kenya $118.1 billion ๐Ÿ‡ฐ๐Ÿ‡ช

5. Angola $117.8 billion ๐Ÿ‡ฆ๐Ÿ‡ด

6. Tanzania $85.4 billion ๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ

7. Cรฒte d'Ivore $77 billion ๐Ÿ‡จ๐Ÿ‡ฎ 

8. DRC $69.4 billion ๐Ÿ‡จ๐Ÿ‡ฉ

9. Ghana $66.6 billion ๐Ÿ‡ฌ๐Ÿ‡ญ

10. Uganda $49.7 billion ๐Ÿ‡บ๐Ÿ‡ฌ

No comments:

Powered by Blogger.