LIVE STREAM ADS

Header Ads

Zaidi ya tani sita za vipodozi zateketezwa na TBS jijini Mwanza

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Zaidi ya tani sita za bidhaa mbalimbali ikiwemo vipodozi vilivyopigwa marufuku kwa matumizi ya binadamu, vimeteketezwa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kufuatilia ukaguzi uliofanywa na maafisa wa shirika hilo kuanzia mwezi Oktoba 2022 hadi Machi 2023 katika mikoa ya Kanda ya Ziwa.

Akizungumza Mei 15, 2023 katika dampo la Buhongwa jijini Mwanza wakati wa zoezi la kuteketeza bidhaa hizo, Meneja wa TBS Kanda ya Ziwa, Happy Kanyeka alisema bidhaa hizo ambazo kama zingekuwa halali zinegkuwa na thamani ya zaidi ya shilingi milioni 100 na kwamba zimekuwa zikiingizwa nchini na kuuzwa kwa kificho na wafanyabiashara wasio waadilifu.

Kanyeka alisema TBS inaendelea kutoa elimu kwa wananchi kuzitambua bidhaa ikiwemo vipodozi vilivyopigwa marufuku ambavyo vina viambata sumu kwani vina madhara makubwa kiafya ikiwemo kusababisha magonjwa ya kansa ambapo hatua hiyo itasaidia kukosa soka na wafanyabiashara kutoshawishika kuviingiza nchini.

Aliongeza kuwa licha ya kwamba TBS imekuwa ikitoa elimu pia kwa wafanyabiashara ili kutoingia sokoni bidhaa hizo, lakini bado wapo wasio waadilifu ambao huziingiza sokoni hivyo zoezi la ukaguzi katika maduka mbalimbali kubaini bidhaa hizo litakuwa endelevu na wanaokamatwa wanachukulia hatua za kisheria ikiwemo kulipa faini, kugharamia uteketezaji wake na kufikishwa mahamakani.

"Kadri ukaguzi unavyofanyika bidhaa hizi zinapungua sokoni hivyo utakuwa ni ukaguzi endelevu huku tukiendelea kutoa elimu kwa wananchi na wafanyabiashara kwani elimu haina mwisho kwani kila siku wafanyabiashara wapya wanaongezeka" alisema Afisa Usalama wa Chakula TBS Kanda ya Ziwa, Nuru Mwasulama.

Mwasulama aliongeza TBS haifurahii kuona wafanyabiashara wanaendelea kupoteza mitaji yao kwa kuingiza sokoni bidhaa zilizopigwa marufuku ndiyo maana inaendelea kuwaelimisha ili kuacha biashara hiyo haramu huku akitoa rai kwa wananchi kuepuka matumizi ya vipodozi vyenye viambatana sumu kwani uzuri unaosababisha madhara kiafya si uzuri hivyo watumie vipodozi halali vilivyosajiliwa na TBS.

Mmoja wa wafanyabiashara jijini Mwanza, January Mkama alisema elimu inayotolewa na TBS itasaidia kutambua aina ya vipodozi halali na kuepuka kuingiza sokoni vipodozi vilivyopigwa marufuku ambavyo huchubua ngozi na kusababisha madhara kwa watumiaji.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Meneja wa TBS Kanda ya Ziwa, Happy Brown Kanyeka akizungumza wakati wa zoezi la kuteketeza bidhaa zilizopigwa marufuku ikiwemo vipodozi.
Meneja wa TBS Kanda ya Ziwa, Happy Brown Kanyeka akizungumza na waandishi wa habari wakati wa zoezi la kuteketeza bidhaa zilizopigwa marufuku ikiwemo vipodozi.
Afisa Usalama wa Chakula TBS Kanda ya Ziwa, Nuru Edgar Mwasulama akitoa taarifa ya zoezi endelevu la ukaguzi wa bidhaa zilizopigwa marufuku ili kuziondoa sokoni.
Afisa Usalama wa Chakula TBS Kanda ya Ziwa, Nuru Edgar Mwasulama akizungumza na waandishi wa habari.
Mmoja wa wafanyabiashara jijini Mwanza, January Mkama akizungumza na wanahabari baada ya kushuhudia zoezi la uteketezaji wa bidhaa zilizopigwa zilikamatwa na TBS katika mikoa ya Kanda ya Ziwa.
Mmoja wa wafanyabiashara jijini Mwanza, January Mkama (kushoto) akizungumza na wanahabari baada ya kushuhudia zoezi la uteketezaji wa bidhaa zilizopigwa zilikamatwa na TBS katika mikoa ya Kanda ya Ziwa.
Maafisa wa TBS Kanda ya Ziwa wakishuhudia zoezi la kuteketeza bidhaa zilizopigwa marufuku ikiwemo vipodozi katika dampo la Buhongwa jijini Mwanza.
Maafisa wa TBS Kanda ya Ziwa wakishuhudia bidhaa zilizokamatwa zikishushwa katika dampo la Buhongwa jijini Mwanza kwa ajili ya kuziteketeza.
Sehemu ya shehena ya vipodozi vilivyopigwa marufuku kuuzwa sokoni ikiwa tayari kuteketezwa.
Shehena ya vipodozi vilivyopigwa marufuku kuuzwa nchini Tanzania.
Katika zoezi hilo, pia aina nyingine ya bidhaa kama mafuta ya kupikia yaliyotengenezwa kiholela bila kuzingatia ubora wa TBS yalimwaga. Pia bidhaa zilizoisha muda kama biskuti na chokoleti ziliteketezwa ikiwa ni hatua muhimu ya kuwalinda walaji.
SOMA PIA>>> Habari zaidi hapa

No comments:

Powered by Blogger.