LIVE STREAM ADS

Header Ads

Jiji la Mwanza lazindua Ripoti ya Mapitio ya Hiari ya SDG's

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Halmashauri ya Jiji la Mwanza imezindua Ripoti ya Mapitio ya Hiari ya Utekelezaji wa Miradi ya Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDG's), iliyoandaliwa kwa ushirikiano baina ya halmashauri hiyo na Halmashauri ya Jiji la Tampere kutoka nchini Finlan pamoja na Shirika la Umoja wa Mataifa la Makazi (UN-HABITAT).

Akipokea na kuzindua ripoti hiyo Jumatatu Juni 12, 2023, Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza Sima Costantine amesema itasaidia kutoa mwongozo wa kushughulikia changamoto za maendeleo endelevu katika nyanja mbalimbali ikiwemo elimu, miundombinu, mazingira, maji safi na salama, ukatili wa kijinsia pamoja na kuimarisha mahusiano baina ya majiji ya Mwanza na Tampere ambayo yamekuwa kwenye ushirikiano tangu mwaka 1988.

Kuhusu uboreshaji wa miundombinu ya makazi, Sima amesema tayari Shirika la Umoja wa Mataifa la Makazi (UN-HABITAT) limeingia makubaliano ya ushirikiano katika mradi wa maendeleo endelevu baina ya Mwanza na Tampere hivyo maeneo ya makazi yaliyoonekana kuwa changamoto ikiwemo makazi ya milimani yanakwenda kuboreshwa zaidi.

"Makubaliano si kuwaondoa wananchi kwenye makazi ya milimani ambayo yalionekana kujengwa kiholela, bali ni kuyaboresha na kuimarisha miundombinu ya huduma mbalimbali ili yavutie kila mtu kukaa hapo ambapo tutashirikiana na UN- Habitant kutekeleza mradi huu" amesema Sima.

Naye Mwakilishi UN- Habitant, Stella Mungai amesema shirika hilo limeridhia kuwezesha utekelezaji wa miradi ya maendeleo endelevu ya ulimwengu (SDG's) ngazi za Halmashauri hatua itakayosaidia jamii na kuhusika kwenye utekelezaji huo na kufikia malengo ifikapo mwaka 2030.
Na George Binagi- GB Pazzo, BMG
Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza Sima Costantine (wa pili kushoto) akipokea Ripoti ya Mapitio ya Hiari ya Utekelezaji wa Miradi ya Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDG's) kutoka kwa viongozi wa majiji ya Mwanza, Tampere na UN- Habitant (kulia) ambapo baada ya upatikanaji wa rasilimali fedha utekelezaji wake utaanza.
Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza Sima Costantine (wa pili kushoto) akipokea Ripoti ya Mapitio ya Hiari ya Utekelezaji wa Miradi ya Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDG's) kutoka kwa viongozi wa majiji ya Mwanza, Tampere na UN- Habitant (kulia).
Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza Sima Costantine akizungumza kwenye hafla hiyo.
Wadau na viongozi mbalimbali wakiwa kwenye uzinduzi wa ripoti hiyo.
Dkt. Mwoya Byato, mshauri
Mratibu wa Mahusiano baina ya Jiji la Mwanza na Tampere, Billy Brown akieleza namna ushirikiano baina ya majiji hayo mawili umesaidia utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo mazingira na kubainisha kuwa ripoti hiyo itasaidia kubaini maeneo yenye changamoto kwa ajili ya kuzitafutia ufumbuzi.
Mwakilishi wa shirika la UN- Habitant, Claudia Garcia akizungumza kwenye hafla ya makabidhiano na uzinduzi wa Ripoti ya Mapitio ya Hiari ya Utekelezaji wa Miradi ya Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDG's) jijini Mwanza.
Mwakilishi wa shirika la UN- Habitant, Stella Mungai akizungumza kwenye hafla ya makabidhiano na uzinduzi wa Ripoti ya Mapitio ya Hiari ya Utekelezaji wa Miradi ya Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDG's) jijini Mwanza.
Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga, Abdulrahman Shiloow akitoa salamu kwenye hafla hiyo ameomba utafiti uliofanyika Mwanza kufanyika pia Tanga ili kusaidia utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo endelevu katika Jiji hilo.
Washiriki wakifuatilia hafla hiyo.
Picha ya pamoja.
Picha ya pamoja.
Picha ya pamoja.
PIA SOMA>>> Habari zaidi hapa

No comments:

Powered by Blogger.