LIVE STREAM ADS

Header Ads

DC Misungwi awataka wananchi kutowaficha wagonjwa ndani

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com 
Mkuu wa Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza, Paulo Chacha amewataka wazazi na walezi wilayani humo kutowaficha ndani watoto wao wenye maradhi mbalimbali yakiwemo ya ulemavu na badala yake wanapaswa kuwafikisha katika huduma za afya kwa ajili ya matibabu.

Chacha alitoa rai hiyo wakati akikabidhi msaada wa shilingi laki nne kwa Mariam Elias mkazi wa Kijiji cha Ikoma kwa ajili ya matibabu ya mwanaye anayesumbuliwa na maradhi ya kichwa kikubwa kwa takribani miaka mitano.
Mkuu wa Wilaya Misungwi mkoani Mwanza, Paul Chacha (kushoto) akimkabidhi Mariam Elias (kulia) kiasi cha shilingi laki nne kwa ajili ya matibabu ya mwanaye Japhet Mitego (aliyebebwa katikati) anayesumbuliwa na maradhi ya kichwa kikubwa.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.