LIVE STREAM ADS

Header Ads

Mapya yaibuka sakata la Kisiwa, Mlima kuuzwa Mwanza

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Mkuu wa Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza, Paul Chacha ametengua maamuzi ya viongozi wa Kijiji cha Kigongo, kuuza Kisiwa katika mwambao wa Ziwa Victoria pamoja na mlima wa mawe na kuagiza kurejesha fedha walizopokea.

Katika sakata hilo, inaelezwa viongozi wa Kijiji hicho wamepokea shilingi milioni 32.6 kama malipo ya mlima kwa ajili ya mwekezaji kupasua mawe huku anayedaiwa kununua kisiwa akitoa shilingi milioni 25 zilizoelekezwa kwenye upauaji wa shule ya Sekondari.
Mwonekano wa kisiwa kilichouzwa katika Kijiji cha Kigongo wilayani Misungwi.
Mwonekano wa mlima wa mawe uliouzwa katika Kijiji cha Kigogo wilayani Misungwi.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Kigongo (kulia) na Mtendaji wa Kijiji hicho (kushoto) wakieleza sakata la kuuza kisiwa pamoja na mlima jinsi lilivyo.
Mkuu wa Wilaya ya Misungwi, Paul Chacha (kulia) akifuatilia sakata la kisiwa na mlima wa mawe kuuzwa katika Kijiji cha Kigongo Kata ya Fella.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.