LIVE STREAM ADS

Header Ads

TASAC yatoa mafunzo kwa Wanahabari Mwanza

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) limetoa mafunzo kwa waandishi wa habari mkoani Mwanza ili kuwajengea uelewa kuhusu shughuli zinazofanywa na shirika hilo kwa ajili ya kuwaelimisha wananchi.

Akizungumza wakati wa mafunzo hayo yaliyofanyika Juni 26, 2023 jijini Mwanza, Kaimu Meneja Masoko na Mahusiano TASAC, Mariam Mwayela alisema waandishi wa habari wakifahamu majukumu yanayofanywa na shirika hilo watasaidia kutoa elimu kwa wananchi.

Alisema TASAC imekuwa ikifanya kazi kwa karibu na waandishi wa habari katika kuelimisha jamii kuhusu sekta ya usafirishaji majini hivyo mafunzo hayo yatawasaidia kufahamu majukumu yanayotekelezwa na shirika hilo na kutoyachanganya na majukumu ya taasisi zingine.

"Hapo awali kulikuwa na changamoto ya kuchanganya shughuli za TASAC na taasisi zingine lakini baada ya mafunzo haya tunaamini mtafanya kazi ya kuelimisha jamii kwa weledi kwani mtakuwa mmeifahamu TASAC na Sheria inazosimamia" alisema Afisa Uhusiano TASAC, Nicholas Kariri wakati akiwasilisha mada kwenye mafunzo hayo.

Baadhi ya washiriki hao akiwemo Bernad James walisema mafunzo hayo yatawasaidia kutimiza vyema majukumu yao ikiwemo kuelimisha watumiaji wa vyombo vya majini kuzingatia usalama kwa kulinda na kutuza vifaa muhimu vya uokoaji ikiwemo maboya.

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) limekuwa na majukumu mbalimbali ikiwemo udhibiti wa usalama na ulinzi wa usafiri majini, ukaguzi na usajili wa vyombo vya majini, kuratibu shughuli za utafutaji na uokoaji majini, utoaji vyeti kwa mabaharia, utoaji wa elimu ya usalama majini, kufanya sensa ya vyombo vya majini pamoja na kuzuia uchafunzi wa mazingira katika mito, maziwa na bahari.
Na George Binagi- GB Pazzo, BMG
Kaimu Meneja Masoko na Mahusiano TASAC, Mariam Mwayela (kulia) wakati wa mafunzo ya kuwajengea uelewa waandishi wa habari mkoani Mwanza.
Afisa Uhusiano TASAC, Nicholas Kariri akiwasilisha mada kwenye mafunzo hayo.
Waandishi wa habari mkoani Mwanza wakifuatilia mada kwenye mafunzo hayo.
Afisa Mahusiano TASAC, Jeffer Matumba akizungumza wakati wa mafunzo hayo.
Waandishi wa habari mkoani Mwanza wakifuatilia mafunzo hayo.
Waandishi wa habari wakifuatilia mada kwenye mafunzo hayo.
Waandishi wa habari mkoani Mwanza wakiwa kwenye mafunzo ya kuwajengea uwezo yaliyoandaliwa na TASAC.
Waandishi wa habari mkoani Mwanza wakifuatilia mafunzo hayo.
PIA SOMA>>> HABARI ZAIDI HAPA

No comments:

Powered by Blogger.