LIVE STREAM ADS

Header Ads

Wadau Mwanza waingia makubaliano na MRBA kuendesha Ligi ya Kikapu 2023/24

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Chama cha Mpira wa Kikapu Mkoa Mwanza (MRBA) kimeingia makubaliano ya ushirikino na wadau wa mchezo huo ambao ni Alphonce Kusekwa, Jeverico Pembe na Evans Liseki ili kuendesha ligi ya MRBA msimu wa mwaka 2023/24 inayotarajiwa kuanza Julai 22, 2023.
Na George Binagi- GB Pazzo, BMG
Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Kikapu Mkoa Mwanza (MRBA), Sunday Mtaki (wa pili kulia) akibadilishana mkataba wa makubaliano na mdau wa mchezo wa Kikapu jijini Mwanza, Alphonce Kusekwa (wa pili kushoto) kwa ajili ya kushirikiana kuendesha ligi ya mchezo huo msimu wa mwaka 2023/24 unaotarajia kuanza Julai 22, 2023.
Anayeshuhudia katikati ni Afisa Michezo Jiji la Mwanza, Mohamed Bitegeko. Wengine kulia na kushoto ni wawakilishi kutoka The Cast Bar & Grill ambayo imeridhia kudhamini ligi hiyo.
Mdau wa mpira wa kikapu ambaye pia ni mchezaji wa mchezo huo, Alphonce Kusekwa (wa pili kushoto) akisaini makubaliano ya kushirikiana na MRBA kuendesha ligi ya mchezo huo msimu wa mwaka 2023/24 inayotarajia kuanza Julai 22, 2023.
Mwenyekiti wa MRBA, Sunday Mtaki (wa pili kulia) akisaini makubaliano ya kushirikiana na wadau wa mchezo wa Kikapu kuendesha ligi ya mchezo huo msimu wa mwaka 2023/24 inayotarajia kuanza Julai 22, 2023. Wadau waliojitoteza kushirikiana na MRBA ni Alphonce Kusekwa, Jeverico Pembe na Evans Liseki.
Picha ya pamoja baada ya zoezi la kusaini makubaliano ya ushirikiano baina ya MRBA na wadau wa mchezo wa kikapu jijini Mwanza.
Picha ya pamoja baada ya zoezi la kusaini makubaliano ya ushirikiano baina ya MRBA na wadau wa mchezo wa kikapu jijini Mwanza.
Picha ya pamoja.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.