LIVE STREAM ADS

Header Ads

Nyamagana wamejipanga kuupokea Mwenge wa Uhuru 2023

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Mapema alfajiri ya Jumamosi Julai 15, 2023 viongozi na wananchi wa Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza wamejitokeza kwa hamasa kubwa katika uwanja wa Shule ya Sekondari Igoma kupokea Mwenge wa Uhuru.

Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Amina Makilagi amejitokeza kuongoza hamasa ya mapokezi ya Mwenge huo uliowasili mkoani Mwanza Julai 13, 2023 ukitokea mkoani Mara.

Ukiwa wilayani Nyamagana, Mwenge wa Uhuru ukiongozwa na Abdalla Shaib Kaim utakagua, kuweka mawe ya msingi na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ya elimu, afya, maji, barabara, uzalishaji mali na mazingira yenye thamani ya shilingi bilioni 4.7 ukikimbizwa umbali wa kilomita 37.7.

Mwenge wa Uhuru unatarajiwa kuhitimisha mbio zake mkoani Mwanza Julai 21, 2023 na kuelekea mkoani Simiyu ambapo kwa mwaka huu kaulimbiu ni "Tunza Mazingira, Okoa Vyanzo vya Maji kwa Ustawi wa Viumbe Hai, Kwa Uchumi wa Taifa".
Na George Binagi- GB Pazzo, BMG 
Tazama picha zaidi hapa chini.
TAZAMA BMG TV HAPA CHINI

No comments:

Powered by Blogger.