LIVE STREAM ADS

Header Ads

Jengo jipya la ghorofa nne kujengwa Hospitali ya Butimba Mwanza

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza, Sima Constantine ameendelea na ziara ya kutembelea na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa na Halmashauri hiyo kwa kuwashirikisha wananchi.

Akizungumza Agosti 14, 2023 baada ya kukagua maandalizi ya ujenzi wa jengo la ghorofa nne katika Hospitali ya Wilaya ya Wilaya Nyamagana Butimba ambalo linaratajiwa kugharimu zaidi ya shilingi bilioni sita, Sima amewataka watumishi wa afya kufanya kazi kwa bidii.

Pia Mstahiki Meya Sima ametumia fursa hiyo kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha za miradi mbalimbali ya maendeleo katika Halmashauri ya Jiji la Mwanza.

"Tunaweza kuwa na majengo mazuri lakini kama hakuna huduma bora hayatakiwa na maana. Shukurani pekee tunayoweza kumpa Mhe. Rais (Dkt. Samia Suluhu Hassan) ni kutoa huduma bora kwa wananchi" amesema Meya Sima akizungumza na watumishi wa hospitali ya Butimba.

Sima pia amekagua ujenzi wa jengo la kuhifadhia maiti katika Hospitali hiyo ambalo tayari limekamilika kwa gharama ya shilingi milioni 149.8 na kuelekeza miundombinu ya jengo hilo ikiwemo barabara kuboreshwa ili kuanza kutoa huduma.

Mradi mwingine aliotembelea Mstahiki Meya Simba ni ujenzi wa jengo la wagonjwa wa nje (OPD) katika Zahanati ya Mkolani ambalo limejengwa kupitia mapato ya ndani kwa kiasi cha shilingi milioni 146.7 ambalo litasaidia kuondoa adha ya msongamano wa wagonjwa katika Zahanati hiyo ambayo inahudumia wagonjwa takribani wagonjwa elfu tano kwa mwaka.
Na George Binagi- GB Pazzo, BMG
Mstahiki Meya Jiji la Mwanza, Sima Costantine (mwenye tai) akiwa katika Hospitali ya Wilaya Nyamagana Butimba kukagua ujenzi wa chumba cha kuhifadhia maiti na maandalizi ya ujenzi wa jengo la huduma mbalimbali ikiwemo dharura, mama na mtoto pamoja na utawala.
Mganga Mfawidhi Hospitali ya Butimba, Dkt. Mohamed Kinawoka (kushoto) akionesha mchoro wa jengo la ghorofa nne linalotarajiwa kujengwa katika hospitali hiyo.
Ujenzi wa jengo hilo ni hatua ya Serikali kuboresha miundombinu ya kutolea huduma katika Hospitali ya Butimba.
Maandalizi ya eneo la ujenzi wa jengo hilo tayari yameanza.
Mwonekano wa jengo la wodi ya wanaume katika Hospitali ya Butimba.
Mwonekano wa jengo jipya la kuhifadhia maiti katika Hospitali ya Wilaya Butimba.
Mwonekano wa jengo jipya la wagonjwa wa nje katika Zahanati ya Mkolani.
Jengo la wagonjwa wa nje (OPD) katika Zahanati ya Mkolani.
SOMA PIA>>> HABARI ZAIDI HAPA

No comments:

Powered by Blogger.