LIVE STREAM ADS

Header Ads

Mafanikio ya Kituo cha Taarifa na Maarifa cha Kivule

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Kituo cha Taarifa na Maarifa cha Kivule kimeelezea mafanikio yaliyojitokeza kutokana na harakati za nguvu ya pamoja na wakishirikiana na Viongozi kwenye kata pamoja na Wananchi walipotembelea na kukagua ufanisi wa miradi hiyo ikiwa na lengo la kuwafikishia wananchi karibu hudama za muhimu.

Afisa Maendeleo Kata ya Kivule, Anna Massawe amesema Kituo hicho kimekuwa na mchango mkubwa sana katika kuibua changamoto hasa zinazotokana na ukatili unaohusisha watoto, wanawake katika sehemu mbalimbali za Kata hiyo.

Amesema pia kimesaidia kupaza sauti katika suala la ukeketaji ambapo Kata ya Kivule ilikuwa ni miongoni mwa Kata zilizokuwa zinaongoza kwa ukatili wa ukeketeji kwa watoto wa kike lakini kwa takribani miaka mitatu sasa kesi hizo zimeisha kabisa na kama zikiwepo hazifanyiki ndani ya kata hiyo, hivyo ikiwa ni faida ya elimu wanayoitoa Kituo hicho hasa kwa sauti zao wanazozitoa mashuleni na kwenye mikutano ya hadhara ndizo zilizosaidia kwa kiasi kikubwa chanamoto hii kuisha katika kata hiyo.

“Nimeweza kupokea watoto wengi wanaokimbia ukeketaji kwamba wengi wamepata uelewa mkubwa kuanzia kwa watoto, wazazi pamoja na jamii kwa ujumla” alisema Afisa Maendeleo

Pia amesema Kituo cha Taarifa na Maarifa cha Kivule kimeweza kuibua migogoro ya ndoa ambayo ilikuwa inasababisha wakinamama wanaonyanyaswa sana mfano vikiwemo vipigo, kunyimwa matumizi ya familia kwani hapo mwanzo hizo changamoto zilikuwa zinafichwa chini ya kapeti lakini kwa sasa zinazungumzwa na wengi wamejua kuwa ni makosa hivyo jamii imeendelea kuelimika.

Pia amesema KC Kivule imehamasha vijana kujiunga kwenye vikundi na mpaka sasa vikundi vya vijana vipatavyo 17 vimeweza kupata mikopo ya Halmashauri na vingine vingi vimeomba ambapo tunasubiria dirisha likifunguliwa wanaweza kupata mikopo hiyo ili kujikimu kimaisha na hamasa ya vijana kujiunga kwenye mikopo imekuwa kubwa katika kata ya Kivule.

Kupitia hamasa walizotumia Kituo cha Taarifa na Maarifa cha Kivule mpaka sasa Mtaa wa Magole wamepata shule kupitia nguvu zao za kuzungumza na wananchi, viongozi hata vyombo vya habari mbalimbali ambapo mwanzo mtaa huo haukuwa na Shule ya Msingi na Sekondari ambapo wanafunzi wengi walikuwa wanatembea umbali mrefu kwenda shule ambapo KC hiyo iliweza kuomba kuingia kwenye vikao vya Kamati ya Maendeleo ya kata na kuingia kwao ndo ilikuwa sehemu sahihi ya kutoa mapendekezo yaliyoleta mafanikio hayo.

Naye Mwenyekiti wa Kituo cha Taarifa na Maarifa cha Kivule, Zahara Mzee amesema kazi kubwa wanaibua changamoto zilizopo kwenye Kata hiyo na kuzichanganua ikiwa nikutafuta vipaumbele ambapo wanaweza kuiwasilisha sehemu husika ili kuweza kutatua changamoto hiyo kwenye Kata ya Kivule.

Amesema Kituo cha Taarifa na Maarifa cha Kivule kinashirikiana na wadau mbalimbali kupitia Afya wanashirikiana na Madaktari, kwenye elimu wanashirikiana na Walimu, Uongozi wa Kata pamoja na Polisi kwasababu kazi hizi wanaibua changamoto tofauti tofauti zikiwepo changamoto za kata husika pamoja na masuala ya ukatili wa kijinsia.

Naye mwanafunzi aliyepitia changamoto ya kupata mimba wakati akiwa kidato cha tatu (jina limehifadhiwa) amesema baada ya kupata ujauzito hakuweza kuendelea na shule na ikampelekea kukaa mwaka mmoja nyumbani lakini kutokana na Kituo cha Taarifa na Maarifa cha Kivule kupata taarifa hiyo waliweza kuwasiana naye na kuweza kumtafutia nafasi ya kuendelea na Shule kupitia mradi wa Mama Samia kupitia Rais wa Awamu ya Sita Dkt. Samia Suluhu Hassan aliweza kupata nafasi ya kuendelea na masomo na mwaka kesho atakuwa anahitimu kidato cha nne katika shule ya Sekondari ya Kitunda
Afisa Maendeleo kata ya Kivule Anna Massawe akizungumza na waandishi wa habari.
Mwenyekiti wa Kituo cha Taarifa na Maarifa cha Kivule, Zahara Mzee.
Afisa Ustawi wa Jamii Hospitali ya Wilaya ya Kivule, Irene Shembilu.
Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Abuuy Jumaa, Froida Mkya.
Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Abuuy Jumaa, Froida Mkya akionesha vyoo vilivojengwa na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan.
Mwonekano wa madarasa mapya manne na vyoo ya Shule ya Sekondari ya Abuuy Jumaa.
Mwenyekiti wa Kituo cha Taarifa na Maarifa cha Kivule, Zahara Mzee akionesha kitolea ufafanuzi baadhi ya majengo ya shule mpya ya Magole inayotarajiwa kuanza hivi karibuni.
Mwenyekiti wa Mtaa wa Magole, Abubakary Kindagule.
Mjumbe wa Kituo cha Taarifa na Maarifa cha Kivule Hamedi Katolela.
Muonekano wa Shule mpya ya Msingi ya Magole iliyopo katika kata ya Kivule.
Mwenyekiti wa Mtaa wa Kivule, Amos Hangaya.
Mwalimu wa Shule ya Msingi Kivule Annex, Joyce Kwambela.
Mwalimu wa Shule ya Msingi Kivule Annex, Joyce Kwambela.
Mkazi wa Kivule, John Mbamba akitoa shukrani kwa Serikali pamoja na Kituo cha Taarifa na Maarifa cha Kivule kwa kuweza kuhamasisha ujenzi wa Barabara kwa kiwango cha lami pamoja na changalawe ambapo wakazi wa Kivule sasa wajivunia na barabara hiyo.
Mwonekano wa barabara iliyopo Kata ya Kivule.

No comments:

Powered by Blogger.