LIVE STREAM ADS

Header Ads

Naibu Meya Jiji la Mwanza asisitiza matumizi sahihi fedha za miradi

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Naibu Meya wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Bhiku Kotecha amesisitiza watendaji wa halmashauri hiyo kuhakikisha wanasimamia vyema fedha za miradi ya maendeleo ili miradi inapokamilika iaksi thamani halisi.

Bhiku ameyasema hayo akizungumza kwa niaba ya Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha ambaye pia ni Mstahiki Meya wa Halmashauri hiyo, wakati wa ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ya elimu.

"Lazima fedha iliyotolewa ifanye kazi iliyokusudiwa, hiyo itatusaidia wakati mwingine kupata fedha zaidi za miradi ya maendeleo" amesema Kotecha huku akimponeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha zaidi ya shilingi bilioni moja kwa ajili ya miradi ya elimu katika Hamlmashauri ya Jiji la Mwanza.

Miongoni mwa miradi iliyokaguliwa na Kamati hiyo ni ujenzi wa shule mpya za awali na msingi Ng'hwang'alanga na Kanenwa ziliyotengewa bajeti ya shilingi milioni 540 kila moja pamoja na ujenzi wa bweni katika shule ya sekondari ya wavulana Nsumba.
Na George Binagi- GB Pazzo, BMG
Mwonekano wa baadhi ya majengo katika shule ya awali na msingi Kanenwa iliyopo Kata ya Kishiri.
Kamati ya Fedha Halmashauri ya Jiji la Mwanza ikikagua miradi ya elimu.
Kamati ya Fedha Halmashauri ya Jiji la Mwanza ikikagua miradi ya elimu.
Kamati ya Fedha Halmashauri ya Jiji la Mwanza ikikagua ujenzi wa shule ya msingi Kanenwa Kata ya Kishiri.
Kamati ya Fedha Halmashauri ya Jiji la Mwanza ikikagua ujenzi wa shule mpya ya Ng'hwang'alanga Kata ya Buhongwa.
Mwonekano wa shule mpya ya awali na msingi Ng'hwang'alanga.
Kamati ya Fedha Halmashauri ya Jiji la Mwanza ikikagua miradi ya elimu.
Kamati ya Fedha Halmashauri ya Jiji la Mwanza ikikagua miundombinu katika shule ya sekondari ya wavulana Nsumba.
Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye ziara ya Kamati ya Fedha kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo.
Kamati ya Fedha Halmashauri ya Jiji la Mwanza ikikagua miundombinu katika shule ya sekondari ya wavulana Nsumba.
Kamati ya Fedha Halmashauri ya Jiji la Mwanza ikikagua miundombinu katika shule ya sekondari ya wavulana Nsumba.
Kamati ya Fedha Halmashauri ya Jiji la Mwanza ikikagua miundombinu katika shule ya sekondari ya wavulana Nsumba.
Kamati ya Fedha Halmashauri ya Jiji la Mwanza ikikagua miundombinu katika shule ya sekondari ya wavulana Nsumba.
Kamati ya Fedha Halmashauri ya Jiji la Mwanza ikikagua miundombinu katika shule ya sekondari ya wavulana Nsumba.
Bweni la wavulana katika shule ya sekondari Nsumba.
Shule ya sekondari ya wavulana Nsumba ilipokea shilingi milioni 245 kwa ajili ya uujenzi wa bweni, vyumba vinne vya madarasa na vyoo matundu sita.

No comments:

Powered by Blogger.