LIVE STREAM ADS

Header Ads

Jiji la Mwanza latakiwa kudhibiti upotevu wa mapato Stendi mpya ya Nyegezi

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Jiji la Mwanza ametakiwa kushughulikia mianya ya upotevu wa mapato katika stendi mpya ya mabasi Nyegezi ambayo tayari imeanza kufanya kazi kwa majaribio tangu Juni 05, 2023.

Ushauri huo umetolea na Kamati ya Huduma za Jamii baada ya kutembelea na kukagua shughuli mbalimbali za uendeshaji wa stendi hiyo ambayo ujenzi wake umegharimu zaidi ya shilingi bilioni 15 hadi kukamilika kwake.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Magreth Kuhanwa amesema ipo mianya ya upotevu wa mapato katika katika stendi ya Nyegezi ikiwemo uwezekano wa tiketi moja kuuzwa kwa mtu zaidi ya mmoja jambo ambalo si sahihi.

"Tumeshuhudia rundo la tiketi zikiwa zimekusanywa bila kuchanwa, hii inaashiria baadae zinauzwa tena kwa abiria wengine wanaoingia humu ndani. Kamati yangu inashauri ufungwe mfumo wa mashine ya ku-scan tiketi. Lakini kwa sasa kwa kuwa bado hakuna mashine, abiria akikata tiketi na kuingia stendi, hiyo tiketi ichanwe" ameshauri Kuhanwa.

Katika hatua nyingine Kuhanwa ameitaka Halmashauri ya Jiji la Mwanza kuhakikisha waliochukua vyumba vya biashara katika stendi hiyo wanaanza kuvitumia kwani asilimia kubwa ya vyumba hivyo bado vimefungwa licha ya kuwa na wapangaji.

Kamati hiyo pia imekagua mradi wa Soko Kuu Mwanza ambao umefikia hatua ya umaliziaji (finishing) na kushauri mkandarasi kuhakikisha anamaliza kazi ya uezekaji ili mradi huo uanze kutoa huduma kwa wananchi.

Miradi mingine iliyokaguliwa na kamati hiyo ni ujenzi wa shule mpya ya awali na msingi Kanenwa Kata ya Kishiri iliyotengewa bajeti ya shilingi milioni 540.3, ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa katika shule ya msingi Bujingwa vilivyotengewa bajeti ya shilingi milioni 81.2 ambapo miradi hiyo iko Kata ya Kishiri.
Na George Binagi- GB Pazzo, BMG 
Mwonekano wa vyumba vitatu vya madarasa mapya katika Shule ya Msingi Bujingwa Kata ya Kishiri jijini Mwanza.
Mwonekano wa Shule ya Msingi Bujingwa.
Wajumbe wa Kamati ya Huduma za Jamii Halmashauri ya Jiji la Mwanza wakiwa kwenye ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo.

Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo.
Wajumbe wa Kamati ya Huduma za Jamii Halmashauri ya Jiji la Mwanza wakiwa kwenye ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo.
Wajumbe wa Kamati ya Huduma za Jamii Halmashauri ya Jiji la Mwanza wakiwa kwenye ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo.
Wajumbe wa Kamati ya Huduma za Jamii Halmashauri ya Jiji la Mwanza wakiwa kwenye ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo.
Wajumbe wa Kamati ya Huduma za Jamii Halmashauri ya Jiji la Mwanza wakiwa kwenye ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo.
Kamati ya Huduma za Jamii Halmashauri ya Jiji la Mwanza ikiwa stendi ya Nyegezi ambapo ilishuhudia tiketi za abiria zilizotumika zikiwa zimekusanywa bila kuchanwa na kuzua hofu ya kuuzwa mara mbili kwa abiria wanaoingia katika stendi hiyo.
Meneja Stendi ya Mabasi Nyegenzi, Madelina Mtweve (kulia) akitoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali ya uendeshaji wa stendi hiyo ambapo amesema tangu ianze kufanya kazi Juni 05, 2023 wamefanikiwa kukusanya mapato zaidi ya shilingi milioni 300 na kwamba changamoto iliyopo ni wapangaji wengi kutoanza kutoa huduma/ kufungua biashara zao.
Wajumbe wa Kamati ya Huduma za Jamii Halmashauri ya Jiji la Mwanza wakiwa kwenye ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo.
Wajumbe wa Kamati ya Huduma za Jamii Halmashauri ya Jiji la Mwanza wakiwa kwenye ziara ya kukagua stendi ya mabasi Nyegezi.
Mwonekano wa mradi wa Soko Kuu Mwanza ukiwa katika hatua ya uezekaji.
Wajumbe wa Kamati ya Huduma za Jamii Halmashauri ya Jiji la Mwanza wakiwa kwenye mradi wa Soko Kuu Mwanza.
Msimamizi wa mradi wa Soko Kuu Mwanza kutoka kampuni ya Mohammed Builders amesema shughuli ya uezekaji itakamilika baada ya bati kuwasili kwani zimeagizwa nje ya nchi baada ya kukosekana ndani ya nchi.
Mwonekano wa vizimba katika Soko Kuu Mwanza.
Mwenyekiti wa Kamati ya Huduma za Jamii kutoka Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Magreth Kuhanwa (katikati) na wajumbe wa kamati hiyo wakikagua mradi wa Soko Kuu Mwanza.
Mwonekano wa mradi wa Soko Kuu Mwanza ukiwa katika hatua ya uezekaji.
Mwonekano wa mradi wa Soko Kuu Mwanza ukiwa katika hatua ya uezekaji.
Mwonekano wa sehemu ya chini (underground) kwa ajili ya maegesho ya magari katika mradi wa Soko Kuu Mwanza.
Mwonekano wa vizimba katika mradi wa Soko Kuu Mwanza.

No comments:

Powered by Blogger.