LIVE STREAM ADS

Header Ads

Wadau wa muziki kukutana jijini Arusha

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanamuziki Tanzania (TAMUFO), Stellah Joel.


Na Dotto Mwaibale, Arusha
Umoja wa Wanamuziki Tanzania (TAMUFO) unatarajia kuwakutanisha wanamuziki, wananchi, viongozi na wadau mbalimbali katika Tamasha kubwa litakalohusu mchango wa wanamuziki katika maendeleo ya nchi ambalo litafanyika kwa siku tatu jijini Arusha.

Akizungumza na waandishi wa habari Katibu Mkuu wa TAMUFO, Stella Joel amesema maandalizi yote yamekamilika na kuwa kwaya mbalimbali na wanamuziki binafsi watakuwepo kutoa burudani.

"Tamasha hilo litakuwa la siku tatu na litafanyika katika Makumbusho ya Taifa ya Elimu Viumbe Arusha jirani na ofisi ya mkuu wa mkoa kuanzia Agosti 25 hadi Agosti 27, 2023" amesema Joel.

Amesema makundi ya kwaya na waimbaji binafsi watakuwepo kutoa burudani wakiongozwa na kwaya Kuu Habari Njema ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) na Kwaya ya Tangazeni ya kanisa hilo Unga Limited zote za jijini Arusha.

Amesema pia kutakuwa na bendi kutoka mikoa mbalimbali ambazo zitashiriki kutoa burudani kwenye tamasha hilo kubwa na la aina yake.

Ametaja kundi lingine ambalo litakuwepo ni wadau wa maendeleo ambapo pia kutakuwepo na fursa mbalimbali na kuwa kiingilio ni bure.

Joel ametumia nafasi hiyo kuwakaribisha wananchi na wadau mbalimbali wa muziki kufika kwenye tamasha hilo ambapo aliwataja baadhi ya wadau watakao kuwepo kuwa ni pamoja na Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Hifadhi |Dodoma ], Dkt.Noelia Myonga, Agness Kanuty, Mwenyekiti wa Nokongo, Dkt. Lilian Badi na Mkurugenzi wa Makumbusho ya Taifa ya Elimu Viumbe Arusha, Dkt. Christina Ngereza.

Mlezi wa TAMUFO Dkt. Frank Richard amesema katika tamasha hilo Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) na COSOTA na TAMRISO watakuwepo kutoa elimu na usajili wa wanamuziki.
Mlezi wa TAMUFO, Dkt. Frank Richard.
Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Hifadhi Dodoma, Dkt.Noelia Myonga.
Mkurugenzi wa Makumbusho ya Taifa ya Elimu Viumbe Arusha, Dkt. Christina Ngereza.

No comments:

Powered by Blogger.