LIVE STREAM ADS

Header Ads

Dola Milioni 300 kutekeleza mradi wa kilimo kwa mfumo wa 'P4R'

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe


Na Nyabaganga Daudi Taraba
Madi wa kilimo umezinduliwa Septemba 06, 2023 kwenye ukumbi mdogo wa Ruaha uliopo katika ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere ikiwa ni sehemu ya shughuli zinazofanyika katika mkutano wa AGRF 2023, Jijini Dar es Salaam.

Mradi huo umejikita katika kutekeleza masuala ya utafiti, ugani, miundombinu na mbegu ili kuwezesha utekelezaji kufanyika.utatekelezwa kwa fedha za mkopo toka banki ya dunia ndani ya miaka mitano

Wanufaika na mradi ni wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na thamani ya mradi ni Dola za Kimarekani milioni mia tatu (300).

Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe amesema inawezekana kabisa fedha hizo zikatumika chini ya miaka mitatu hii ni kutokana na uhitaji uliopo., hivyo, amewaomba wadau husika katika masuala ya fedha kumpa ushirikiano ili mradi utekelezwe na kukamilika mapema.

Aidha amewaomba wakuu wa mikoa kuhakikisha kuwa mradi unatekelezwa, maana wao ndio wana watu na ardhi.

Amewaasa wananchi kuacha kuita wakulima kuwa ni wakulima wadogo, maana huo udogo umepimwa na kipimo gani? kipimo gani kinachotumika kuwapima ili kuwaita wadogo. Kufanya hivyo ni kuendelea kuupa umaskini nguvu.

Waziri Bashe amesema kama P4R imewezekana katika ujenzi wa madarasa, katika kilimo pia itawezekana.

No comments:

Powered by Blogger.