LIVE STREAM ADS

Header Ads

Shirika la EMEDO lautambulisha mradi wa 'kuzuia kuzama maji' kwa waandishi wa habari

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Shirika la Usimamizi wa Mazingira na Maendeleo (EMEDO) limekutana na waandishi wa habari wanaoandika habari za uvuvi (TMFD) kwa ajili ya kuwajengea uelewa kuhusu mradi wa kuzuia kuzama maji unaolenga kuzuia vifo katika maziwa mbalimbali ikiwemo Ziwa Victoria.

Warsha hiyo imefanyika Septemba 06, 2023 jijini Dodoma ikijumuisha washiriki kutoka mikoa mbalimbali ikiwemo Mwanza, Geita, Pwani na Dar es salaam.
Na George Binagi- GB Pazzo, BMG
Mjumbe wa Bodi ya EMEDO, Edwin Soko akiunua mafunzo hayo.
Mjumbe wa Bodi ya EMEDO, Edwin Soko akizunumza wakati wa mafunzo hayo.
Meneja mradi wa kuzuia kuzama maji Ziwa Victoria. Arthur Mugema akizungumza wakati wa mafunzo ya kuutambulisha mradi huo kwa waandishi wa habari yaliyofanyika jijini Dodoma.
Meneja mradi wa kuzuia kuzama maji Ziwa Victoria. Arthur Mugema akizungumza wakati wa mafunzo ya kuutambulisha mradi huo kwa waandishi wa habari.
Meneja mradi wa kuzuia kuzama maji Ziwa Victoria. Arthur Mugema akizungumza wakati wa mafunzo ya kuutambulisha mradi huo kwa waandishi wa habari yaliyofanyika jijini Dodoma.
Mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo, George Binagi kutoka BMG akichangia hoja.
Mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo, Alphonce Tonny kutoka MPC akichangia mada.
Mshiriki Joel Maduka kutoka ETV akichangia mada kwenye mafunzo hayo.
Washiriki wakiwa kwenye mafunzo.
Washiriki wakiwa kwenye maunzo hayo.
Washiriki wakiwa kwenye mafunzo hayo.
Washiriki wakiwa kwenye picha ya pamoja.
Washiriki wakiwa kwenye picha ya pamoja.
Washiriki wakiwa kwenye picha ya pamoja.
Mradi wa kuzuia kuzama maji ziwa Victoria unaotekelezwa na Taasisi ya Usimamizi wa Mazingira na maendeleo ya kiuchumi ( Emedo ) katika mikoa mitatu ya Mwanza, Kagera na Mara, umeanza kutoa elimu kwa waandishi wa habari ili wawe chachu katika kuleta mabadiliko ya kifikra kwenye jamii na kuibua changamoto zinazotishia usalama wa wavuvi nchini.

Mradi huo wa miaka mitatu unaofadhiliwa na Shirika la Royal National Lifeboat Institute la Uingereza unalenga kuvifikia vijiji saba vya wilaya za Muleba, Ukerewe, Nyamagana na Musoma vijijini.

Meneja mradi wa kuzuia kuzama maji Ziwa Victoria Arthur Mugema akizungumza jijini Dodoma, amesema walengwa wakubwa wa mradi huo unaotekelezwa kuanzia mwaka 2022 -2025 ni wavuvi, akinamama wanaochakata mazao ya samaki na watoto wadogo wanaoishi kwenye maeneo ya uvuvi kwenye vijiji vya mradi huo.
Mratibu wa mtandao wa kitaifa wa kuzuia kuzama maji Tanzania Mary Francis amesema lengo la mradi huo ni kuishawishi Serikali iweze kutengeneza sera na mipango ambayo itasaidia kupunguza vifo vya kuzama maji kwa wavuvi na wananchi wengine kwa ujumla.

Mjumbe wa Bodi ya Emedo Edwin Soko amesema eneo la uandishi wa habari za masuala ya kuzama maji bado halijapewa umuhimu unaohitajika, hivyo amewashauri wanahabari kutumia kalamu zao kuandika habari hizo kwa kuzingatia misingi ya maadili ya taaluma yao na kwa weledi mkubwa.

Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo Benard James pamoja na Gloria Kiwia wameushauri mradi huo kuwekeza pia katika eneo la kutoa mafunzo ya namna ya kuogelea pamoja na kuwapatia vifaa vya kujiokoa pindi yanapotokea majanga ya kuzama maji.
PIA SOMA>>> HABARI ZAIDI HAPA

No comments:

Powered by Blogger.