LIVE STREAM ADS

Header Ads

Serikali yaanza kununua dhahabu

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Serikali kupitia Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imeanza mpango maalum wa ununuzi wa Madini ya dhahabu kwa lengo la kuongeza akiba ya nchi ya fedha za kigeni.

Hayo yameelezwa na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko wakati akifungua Maonesho ya Sita (6) ya Teknolojia ya Madini yanayoendelea mkoani Geita.

Dkt.Biteko ameipongeza Benki Kuu ya Tanzania kwa kuanza mpango wa ununuzi wa Madini ya dhahabu na kuhifadhi ambapo mpaka sasa BoT imenunua kiasi cha kilogram 418 za dhahabu yenye kiwango cha asilimia 99.9.

Akizungumza kuhusu mpango huo Dkt. Biteko amesema kuwa BoT imepanga kununua kiasi cha Tani sita kutoka kwa wachimbaji na wauzaji wa Madini nchini.

Vilevile kuhusu maendeleo ya Sekta Madini, amesema uwepo wa viwanda vizuri vyenye teknolojia ya kisasa katika uchakataji na usafishaji wa madini ya dhahabu ndani ya nchi kumepelekea kujenga imani kwa wanunuzi mbalimbali akiwemo BoT tofauti na awali kabla ya kuwepo kwa viwanda uchakataji na usafishaji kufikia kiwango cha asilimia 99.9.

Akielezea juu ya mpango huo Dkt. Biteko ameelekeza kuwa ni vyema kuwepo na mkakati mzuri wa kuwafiki wachimbaji wadogo popote watakapo chimba ili wauze dhahabu kwa uwazi na bei itakayoendana na soko la Dunia kukifanyika hivyo kutaondoa mawazo ya utorosha wa Madini.

Pia ameelekeza kuundwa Kanuni mpya za uchenjuaji Madini ili wachenjuaji waweze kufanya kazi zao kwa imani na uhakika kwa kufuata hizo kanuni zitakazo undwa.

Akizungumza kuhusu Vision 2030 ni Maisha na Utajiri , Dkt. Biteko amesema kuwa mpango wa Serikali ni kuwa ifikapo 2025 sekta ya Madini ichangie asilimia 10 katika pato la taifa hivyo juhudi zifanyike katika ukusanya mapato.

Sambamba na hapo amewaelekeza Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kutoa elimu kwa wachimbaji wadogo wa Madini juu ya malipo ya asilimia mbili (2%) kwa wachimbaji wadogo katika uzalishaji wao ili wapate elimu hiyo na kuona umuhimu wa kulipa kodi husika.

No comments:

Powered by Blogger.