LIVE STREAM ADS

Header Ads

Vijana Shinyanga wanufaika na elimu ya afya ya uzazi

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Mwezeshaji Rika, Martha Salehe mkazi wa Kishapu wilayani Kahama amesema kupitia mradi wa USAID Afya Yangu- RMNCAR, vijana wamenufaika na elimu ya afya ya uzazi na hivyo kuepukana na hatari mbalimbali ikiwemo magonjwa ya zinaa kwani msisitizo mkubwa kwao ni kujiepusha na vitendo vya ngono katika umri mdogo na badala yake wajitunze hadi watakapoanzisha familia.
Mwelimishaji Rika, Dotto Kasiga kutoka Ushetu wilayani Kahama amesema kupitia vikundi vya vijana katika Kata za Chona, Ulowa na Ukune wamekuwa wakihamasisha vijana kujitunza na kutumia ujuzi walio nao kujipatia kipato.
Mmoja wa wanafunzi wa Shule ya Sekondari Dakama iliyopo Ushetu wilayani Kahama, Hellen Peter amesema zipo athari ikiwa vijana hawatapewa elimu mapema kuhusu umuhimu wa afya ya uzazi ambapo elimu hiyo inawasaidia kujilinda ili kutimiza ndoto yao kielimu.
Mmoja wa wanafunzi wa Shule ya Sekondari Dakama iliyopo Ushetu wilayani Kahama, Queen Raphael amesema kupitia midahalo mbalimbali ya vijana, amepata elimu iliyomsaidia kujitambua na sasa anawaelimisha vijana wenzake ndani na nje ya shule kujitunza ili kufikia malengo yao.
Mwalimu wa Shule ya Sekondari Dakama iliyopo Halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama, Mwl. Samwel Biseko elimu ya afya ya uzazi inayotolewa kwa vijana inawasaidia kujitunza na kujikinga na athari za magonjwa ya zinaa.
***

Na George Binagi- GB Pazzo, BMG
Vijana wamenufaika na elimu ya afya ya uzazi katika Halmashauri za Shinyanga Mjini pamoja na Ushetu mkoani Shinyanga kupitia mradi wa USAID Afya Yangu- RMNCAR katika kipindi cha mwaka 2022/23.

Katika Halmashauri ya Shinyanga Mji mradi huo unatekelezwa katika Kata mbili za Samuye na Salawe huku Halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama ukitekelezwa katika Kata tatu za Chona, Ulowa na Ukune.

Miongoni mwa elimu wanayonufaika na vijana waliofikiwa na mradi huo ni pamoja na kujiepusha na vitendo vya ngono katika umri mdogo ili kuepuka hatari ya kupata maradhi ya zinaa, HIV/ UKIMWI pamoja na vitendo vya ukatili wa kijinsia.

Mratibu Msaidizi Afya, Uzazi, Mama na Mtoto Mkoa wa Shinyanga, Hellen Kasakenta amesema vijana wakipata elimu hiyo itawasaidia kujiepusha na vishawishi mbalimbali na hivyo kufikia malengo yao ikiwemo kuhitimu masomo salama na kutimiza malengo yao maishani.

"Unapokuwa kijana, vishawishi ni vingi hivyo wanafundishwa juu ya elimuya afya ya uzazi ili waweze kujikinga, kutulia na kuepuka vishawishi ili waweze kutimiza ndoto zao" amesema Kasakenta.

Mwanafunzi Queen Kiami ambaye ni mmoja wa vijana waliofikiwa na elimu hiyo amesema elimu aliyoipata imemsaidia yeye na wenzake kujiepusha na makundi hatarishi ambayo ni hatari katika maisha yao ya kimasomo hatua ambapo imewanusuru pia wanafunzi kuacha shule.

Kwa upande wao, Mwalimu Samwel Biseko na Mwalimu Leah Msyani kutoka Shule ya Sekondari Dakama Halmashauri ya Ushetu wamesema mradi wa USAID Afya Yangu- RMNCAH umerahisha ufundishaji wa elimu ya afya kwa vijana wakiwemo wanafunzi wa Sekondari hatua ambao imepunguza utoro kwani wamejitambua na kuepuka makundi hatarishi. 

Elimu hiyo inayotolewa kupitia midahalo mbalimbali inayofanyika ndani na nje ya shule za Sekondari katika Kata zinazotekeleza mradi wa USAID Afya Yangu- RMNCAH unaotekelezwa kwa miaka mitangu kuanzia mwaka 2022/27.
PIA SOMA>>> Huduma za Afya

No comments:

Powered by Blogger.