Tanzania kuboresha mfumo wa usimamizi na utoaji taarifa za anga
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Mkurugenzi Mkuu wa TCAA- Hamza Johari (katikati), Mkurugenzi Huduma za Sheria TCAA- Maria Makala (wa pili kulia), Mwakilishi wa kampuni ya Indra Avitech- Simon Masike (wa pili kushoto) wakisani kandarasi ya mkataba wa utekelezaji wa mradi wa mfumo wa usimamizi na utoaji wa taarifa za anga wenye thamani Bilioni Tisa katika hafla iliyofanyika Makao Makuu ya TCAA- Septemba 22, 2023.
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), imesaini kandarasi ya mfumo wa usimamizi wa taarifa za anga na kampuni ya Indra Avitech kwa ajili ya kuboresha usalama wa safari angani katika anga ya Tanzania kupitia utoaji wa taarifa za anga zenye ubora wa hali ya juu, salama na muhimu kwa wakati sahihi kwa wadau mbalimbali wa usafiri wa anga.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Hamza Johari amesema mamlaka hiyo imesaini mkataba wenye thamani ya Shilingi bilioni tisa kwa ajili ya kubuni, kusambaza, kusanikisha, kuunganisha, na kuzindua mfumo wa usimamizi wa taarifa za anga ambapo mradi huo utatekelezwa kwa miezi 18.
Amesema ni sehemu ya mpango thabiti wa usimamizi wa taarifa za anga (AIM) wa kuboresha mfumo wake wa taarifa za anga kwa kutoa usimamizi wa taarifa za anga kwa njia ya kisasa zaidi kwa kutoa na kubadilishana taarifa za anga za dijitali zenye ubora na kushirikiana na pande zote hivyo kuhakikisha usalama, utaratibu na ufanisi wa usambazaji wa anga wa kitaifa na kimataifa.
“Lengo la utekelezaji wa mradi wa mfumo wa usimamizi wa taarifa za anga ni kuboresha mfumo wa AIM katika kuboresha usahihi wa data, upatikanaji, na ufanisi kwa kuzingatia mahitaji ya upandishaji wa mfumo wa anga wa usafiri (ASBU) na kufuata viwango vya kitaifa na kimataifa” amesema Johari.
Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Hamza Johari (wa pili kushoto) akikabidhiana mkataba na Mwakilishi wa kampuni ya Indra Avitech, Simon Masike baada ya kusaini kandarasi ya utekelezaji wa mradi wa mfumo wa usimamizi na utoaji taarifa za anga na kampuni ya Indra Avitech wenye thamani ya shilingi bilioni tisa. Wa pili kulia ni Mkurugenzi Huduma za Sheria TCAA, Maria Makala.
Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Hamza Johari (katikati) na Mwakilishi wa kampuni ya Indra Avitech, Simon Masike (wa pili kushoto) wakionesha mkataba wa makubaliano baada ya kusainiwa na pande zote mbili.
Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Hamza Johari (katikati) akizungumza kwenye hafla hiyo.
Mwakilishi wa kampuni ya Indra Avitech, Simon Masike akizungumza kwenye hafla hiyo.
Kaimu Mkurugenzi Wa Huduma Za Uongozaji Ndege TCAA, Hamis Kisesa akizungumza kwenye hafla hiyo.
Mkurugenzi wa Idara ya Udhibiti Uchumi TCAA- Daniel Malanga (katikati), Mkurugenzi wa Huduma za Mamlaka- Teophory Mbilinyi (kushoto) na Mkurugenzi Huduma za Sheria TCAA, Maria Makala wakiwa kwenye hafla hiyo.
Meneja Uhusiano na Mawasiliano TCAA- Yessaya Mwakifulefule (kushoto), Mkuu wa Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC)- Aristid Kanje (katikati) na Afisa Mtoa Taarifa za Anga Mwandamizi (TCAA) wakiwa kwenye hafla ya kusaini mkatabata huo.
Baadhi ya wadau mbalimbali wa usafiri wa anga wakiwa kwenye hafla ya kusaini mkatabata huo.
Picha za pamoja.
No comments: