LIVE STREAM ADS

Header Ads

UWT Kahama watemebelea bungeni jijini Dodoma

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Mbunge wa viti Maalum Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Lucy Mayenga amewakabidhi Makatibu na Wenyeviti wa Umoja wa Wanawake CCM (UWT) wa Kata 112 kutoka wilaya ya Kahama shilingi milioni 11.2 kwa ajili ya programu ya kuongeza Marafiki wa Chama Cha Mapinduzi sambamba na kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuwaletea maendeleo wananchi wa Mkoa wa Shinyanga na nchi nzima.

Programu hiyo imezinduliwa Alhamisi Septemba 07,2023 na Lucy Mayenga jijini Dodoma baada ya Makatibu na Wenyeviti wa UWT kutoka Kata 112 kutoka wilaya ya Kahama kuwasili mkoani Dodoma kwa mwaliko wake ambapo viongozi hao wamepata nafasi ya kutembelea Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Tukio la uzinduzi wa Programu hiyo pia limehudhuriwa na viongozi wengine wakiwemo Mbunge wa jimbo la Msalala Idd Kassim, Mbunge wa Jimbo la Kahama Jumanne Kishimba, Mbunge wa jimbo la Ushetu Emmanuel Cherehani, Mbunge wa Viti Maalum Chadema Salome Makamba, Naibu Waziri wa Nishati Judith Kapinga, Mbunge wa Viti Maalum Mtwara Agnes Hokororo na Mbunge wa jimbo la Nyang'wale Hussein Nassor.

No comments:

Powered by Blogger.