LIVE STREAM ADS

Header Ads

Jambo Super League kutimua vumbi Shinyanga

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Meneja Rasilimali Watu, Utawala na Sheria wa Kampuni ya Jambo Group, Wakili John Palamagamba Kabudi akizungumza na Vyombo vya Habari Jumamosi Oktoba 28, 2023.
Meneja Rasilimali Watu, Utawala na Sheria wa kampuni ya Jambo Group, Wakili John Palamagamba Kabudi akikabidhi jezi kwa timu zinatakazoshiriki Jambo Super League.

Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Michuano ya Ligi ya Jambo ‘Jambo Super League’ inayohusisha Timu 10 za Wafanyakazi kutoka Idara mbalimbali katika Kampuni ya Jambo Group (Jambo Group of Companies) itaanza kutimua vumbi kesho Jumapili Oktoba 29,2023 katika uwanja wa Chuo cha Ualimu Shinyanga (Shycom) Mjini Shinyanga.

Akizungumza na vyombo vya habari jumamosi Oktoba 28, 2023, Meneja Rasilimali Watu, Utawala na Sheria wa kampuni ya Jambo Group, Wakili John Palamagamba Kabudi amesema mshindi wa kwanza katika kigi hiyo ataondoka na kitita cha shilingi milioni mbili, kombe na medali huku mshindi wa pili akiondoka na shilingi milioni 1.8 na medali wakati mshindi wa tatu akipata shilingi milioni moja.

“Jambo Super League itaanza Jumapili Oktoba 29, 2023 saa nane mchana katika uwanja wa Shycom na watakaotufungulia kesho ni timu ya Jambo Store na Jambo Transport, mechi ya pili itakayoanza saa 10 jioni ni kati ya Jambo Biscuit na Jambo Plastic ambayo itafanyika hapo hapo Shycom” amesema Kabudi.

Ameeleza kuwa mechi zote zitachezwa kila Jumapili kwa muda wa wiki saba kuanzia Oktoba 29, 2023 hadi Desemba 17, 2023 ikihusisha timu 10 za mpira wa miguu za zafanyakazi wa kampuni ya Jambo Group kutoka idara mbalimbali ambazo ni Ice Cream, CSD, Biscuit, Store, Jambo Media & Administration, Plastic, Zoo, Garage, Bakery na Printing.

“Viwanda vyetu ni vingi, lengo la ligi hii ni kuwaleta pamoja wafanyakazi wa kampuni ya Jambo Group ili kufahamiana, tujuane, tufanye mazoezi pamoja kwa sababu nusu ya siku tunaitumia hapa kama ndugu. Kila mwaka tumekuwa tukiwaleta wafanyakazi pamoja kwa namna tofauti. Lakini mwaka huu tumeona tuwalete pamoja kimichezo ili humo wapate pia afya, tugundue vipaji vingine pengine siku moja tutakuwa na timu ya mpira ya Jambo FC/ Jamukaya itakayoshiriki ligi ngazi ya wilaya, mkoa na ligi kuu” ameongeza Kabudi.

“Nitumie fursa hii kuwaomba wadau wote wajitokeze kuunga mkono juhudi za Wafanyakazi na Kampuni ya Jambo Group kuwaleta wafanyakazi pamoja, kufurahi pamoja na kufanya mazoezi pamoja” amesema.

Pia Kabudi ametambulisha kamati yenye wajumbe wasiopungua watano ambapo mmoja wao atatoka Chama Cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Shinyanga, kamati ya maamuzi, huduma ya kwanza, kitengo cha michezo Jambo Media na kukabidhi jezi kwa timu zinazoshiriki ligi hiyo ya Jambo Super League.
Meneja Rasilimali Watu, Utawala na Sheria wa kampuni ya Jambo Group, Wakili John Palamagamba Kabudi akizungumza na vyombo vya habari Jumamosi Oktoba 28,2023.
Meneja Rasilimali Watu, Utawala na Sheria wa kampuni ya Jambo Group, Wakili John Palamagamba Kabudi akionesha moja ya jezi zitakazotumika katika Jambo Super League.
Meneja Rasilimali Watu, Utawala na Sheria wa kampuni ya Jambo Group, Wakili John Palamagamba Kabudi akionesha moja ya jezi zitakazotumika katika Jambo Super League.
Meneja Rasilimali Watu, Utawala na Sheria wa kampuni ya Jambo Group, Wakili John Palamagamba Kabudi akionesha moja ya jezi zitakazotumika katika Jambo Super League.
Meneja Rasilimali Watu, Utawala na Sheria wa kampuni ya Jambo Group, Wakili John Palamagamba Kabudi akikabidhi jezi kwa timu zinatakazoshiriki Jambo Super League.
Meneja Rasilimali Watu, Utawala na Sheria wa kampuni ya Jambo Group, Wakili John Palamagamba Kabudi akikabidhi jezi kwa timu zinatakazoshiriki Jambo Super League.
Meneja Rasilimali Watu, Utawala na Sheria wa kampuni ya Jambo Group, Wakili John Palamagamba Kabudi akikabidhi jezi kwa timu zinatakazoshiriki Jambo Super League.
Meneja Rasilimali Watu, Utawala na Sheria wa kampuni ya Jambo Group, Wakili John Palamagamba Kabudi akikabidhi jezi kwa timu zinatakazoshiriki Jambo Super League.
Meneja Rasilimali Watu, Utawala na Sheria wa kampuni ya Jambo Group, Wakili John Palamagamba Kabudi akikabidhi jezi kwa timu zinatakazoshiriki Jambo Super League.
Meneja Rasilimali Watu, Utawala na Sheria wa kampuni ya Jambo Group, Wakili John Palamagamba Kabudi akikabidhi jezi kwa timu zinatakazoshiriki Jambo Super League.

No comments:

Powered by Blogger.