LIVE STREAM ADS

Header Ads

Kada wa CCM akabidhi kiwanja kwa wana CCM Singida

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Mandewa Hamis Shabani Msabaha (maarufu kama Muna Dalali), ambaye alikuwa mgeni rasmi akizungumza na wana CCM wa Mtaa wa Unyika katika mkutano mkuu wa Tawi hilo uliofanyika Oktoba 06, 2023.


Na Dotto Mwaibale, Singida
Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Mandewa Hamis Shabani Msabaha (maarufu kama Muna Dalali) amekabidhi Kiwanja chenye thamani ya Sh.Milioni 3 kwa wanachama wenzake wa CCM wa Tawi la Unyinga Kata ya Mandewa Manispaa ya Singida mkoani hapa.

Msabaha ambaye ni mjumbe wa kamati ya siasa ya Kata ya Mandewa, mjumbe wa mkutano mkuu Wilaya ya Singida Mjini na Mlezi wa CCM Tawi la Unyinga amefikia hatua hiyo kutokana na mapenzi yake binafsi kwa CCM na maono chanya katika kuhakikisha chama hicho chini ya Mwenyekiti wake Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kinaendelea kustawi kwa manufaa ya watanzania.

Akizungumza katika mkutano mkuu wa chama hicho Tawi la Unyinga ambapo amepokea taarifa ya chama aliwataka wana CCM kujenga tabia ya kujitoa na kuhakikisha ilani ya CCM inatekelezwa ipasavyo.

Mbali ya kutoa kiwanja hicho Msabaha ameshiriki chakula cha pamoja na kutoa misaada kwa wazee wasiojiweza na kwa wajumbe wenzake mbalimbali kama ishara ya upendo na ushirikiano lengo likiwa ni kuleta maendeleo katika tawi hilo na Singida kwa ujumla.

Aidha Msabaha ametoa saruji mifuko 150 kwa ajili ya kuanza kujenga msingi wa ofisi hiyo na akawaomba wana CCM wenzake kujitoa ili kukamilisha ofisi hiyo na kuanza kutumika katika muda mfupi ujao.

Baadhi ya watu waliohudhuria shughuli hiyo akiwamo Mwenyekiti wa Kijiji cha Mandewa, Omari Said, wamemshukuru Msabaha kwa kuwa na moyo wa kujitoa kusaidia shughuli mbalimbali za kijamii na akaomba watu wengine kuiga tabia hiyo.

Katika mkutano huo Mashujaa wa Maendeleo na Ustawi wa Jamii Tanzania (SMAUJATA) Kata ya Mandewa wakiongozwa na Mwenyekiti wa Mkoa wa Smaujata, Idara ya Uhitaji, Maafa na Makundi maalumu, Ramadhani Mdanku walipata fursa ya kuelezea ukatili wa kijinsia na kukithiri kwa vitendo vya watoto wa kiume kulawitiwa na hatua ambazo zinapaswa kuchukuliwa kwa wazazi na walezi ili kukabiliana na vitendo hivyo.

Mkuu wa Polisi Kata ya Mandewa, Mkaguzi wa Polisi Ramadhani Hemba amewahimiza wazazi na walezi kusimamia malezi ya watoto wao na kueleza vitendo vya ukatili dhidi ya watoto hasa kulawitiwa watoto wa kiume vimezidi kuongezeka na wahusika wakiwa ni ndugu au jamaa wa karibu wa waathirika hao.

Hemba ametoa wito kwa jamii kutoa taarifa mara moja pale watakapoona vitendo hivyo ili sheria ichukue mkondo wake au wapige simu bure namba 116.

"Serikali imeshusha huduma za Jeshi la Polisi hadi ngazi ya chini kabisa kwenye kata kwa ajili ya kuwasaidia wananchi hivyo msiogope kutoa taarifa za kihalifu ili muweze kusaidiwa kwani sisi polisi ndio wenye wajibu wa kushirikiana na ninyi katika kukabiliana na vitendo hivyo" amesema Hemba.
Mwenyekiti wa CCM Tawi la Unyinga, Athumani Hango akizungumza kwenye mkutano huo.
Mwenyekiti wa Mkoa wa Smaujata, Idara ya Uhitaji, Maafa na Makundi maalumu, Ramadhani Mdanku, akizungumza kwenye mkutano huo.
Mkuu wa Polisi Kata ya Mandewa, Mkaguzi wa Polisi Ramadhani Hemba, akizungumzia vitendo vya ukatili kukithiri na hatua za kuchukua hasa malezi mema kwa watoto.
Mkutano ukiendelea.
Katibu wa UVCCM Kata ya Mandewa, Yusuph Nkii, akizungumza.
Kikundi cha utamaduni cha Misake kikitumbuiza.
Mkutano ukiendelea.
Mkutano na taaifa mbalimbali zikitolewa.
Viongozi wakiwa jukwaa kuu.
Wasanii wa kundi la makhirikhiri wakionesha umahiri wa kucheza sarakasi.
Viongozi wakitoa nasaha zao kwenye mkutano huo.
Watoto wakiwa kwenye mkutano huo.
Mashujaa wa Smaujata Kata ya Mandewa wakiimba shairi kwenye mkutano huo. Kutoka kushoto ni Mjumbe wa kamati ya utekelezaji ya CCM Wilaya ya Singida mjini, Asha Juma na Mwenyekiti wa Smaujata Kata ya Mandewa, Mwajuma Mikindo.
Wanawake wakiwa kwenye mkutano huo.
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Unyinga akichangia jambo alitoa angalizo wa vitendo vya wizi ambavyo vimeanza kuchipua katika eneo hilo.
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Kijiji cha Mandewa, Omari Said akizungumza.
Mwenyekiti wa Smaujata Kata ya Mandewa Ibrahim Sombi akizungumza.
Mjumbe wa kamati ya utekelezaji ya CCM Wilaya ya Singida mjini, Asha Juma, akizungumza.
Mgeni rasmi Hamis Msabaha, akitoa mchele kwa wakina mama.
Mgeni rasmi Hamis Msabaha akitoa mchele kwa wazee wasiojiweza.
Chakula kikitolewa kwa wenye uhitaji.
Taswira ya mkutano huo.
Viongozi wakiwa katika picha ya pamoja katika mkutano huo.
Mgeni rasmi akiwa katika picha ya pamoja na wazee baada ya kuwapa msaada wa chakula.
Mgeni rasmi Hamis Msabaha (maarufu kama Muna Dalali na Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya CCM Wilaya ya Singida mjini, Asha Juma wakionesha umahiri wa kupiga kwata baada ya mkutano huo kumalizika.

No comments:

Powered by Blogger.