LIVE STREAM ADS

Header Ads

NSSF Singida yatambua vinara wa michango ya wanachama

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Meneja wa NSSF Mkoa wa Singida, Oscar Kalimilwa (katikati)Sr Franca Ogbunuju kutoka Shirika la Srs Medical Missionaries of Mary (MMM), (kulia) na Mwakilishi wa Kanisa la Evangelist Assemblies of God Tanzania (EAGT) Kiomboi Iramba John Leonard wakikata keki maalumu kwa ajili ya maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja yaliyoandaliwa na NSSF Oktoba 06, 2023,

Na Dotto Mwaibale, Singida
Wakati maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja yakiadhimishwa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Mkoa wa Singida limezitambua taasisi na kuwashukuru waajiri wanaojitolea kwa hali na mali kuhakikisha michango ya wanachama wake inawasilishwa kwa wakati.

Hata hivyo shirika hilo pamoja na mambo mengine limezitaja taasisi takribani tano zilizoongoza kwa uwasilishaji wa michango hiyo kwa mwaka huu mkoani hapa zikiwemo Mount Meru Miller na Tree for the Future.

Nyingine ni Makiungu Hospital, Srs Medical Missionaries of Mary (MMM) na Kanisa la Evangelist Assemblies of God Tanzania (EAGT) Kiomboi Iramba ambazo zimetunukiwa vyeti vya kutambua mchango huo.

Hata hivyo akizungumza wakati wa utoaji wa vyeti hivyo Meneja wa NSSF Mkoa wa Singida, Oscar Kalimilwa ameanisha sababu za utoaji wa tuzo hizo kuwa taasisi hizo zimekuwa zikitekeleza sheria za NSSF kwa kupeleka michango na kuandikisha wanachama kwa wakati.

"Wapo waajiri wakubwa na wadogo wenye michango mikubwa kabisa na wenye michango midogo lakini hawa wamefanya vizuri zaidi" amesema Kalimilwa.

Kalimilwa amehimiza waajiri kufuata sheria za NSSF na kuwataka kutekeleza takwa hilo la kisheria kwa mustakabari wa maslahi bora ya wafanyakazi wao pindi wanapo staafu.

Baadhi ya waajiri waliopata vyeti hivyo, Otomali Haule kutoka Hospitali ya Makiungu, Sr Franca Ogbunuju kutoka Shirika la Srs Medical Missionaries of Mary (MMM), waliishukuru NSSF kwa kutambua mchango na kuwa mafanikio hayo yametokana na ushirikiano uliopo baina ya pande zote mbili ambapo walitoa wito kwa taasisi zingine kujenga tabia ya kupeleka michango yao katika mfuko huo.

Tukio hilo la kuzitunuku vyeti vya heshima taasisi hizo limeambatana na kilele cha maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja kwa mwaka 2023 ambayo yamebeba ujumbe usemao ‘Ushirikiano kwa Huduma Bora, ‘Team work for service Excellency’.
Wawakilishi wa taasisi zilizofanya vizuri wakiwa kwenye maadhimisho hayo.
Mwakilishi wa Shirika la Tree for the Future. Frank Marley akilishwa keki.
Keki ikiliwa.
Sr Franca Ogbunuju kutoka Shirika la Srs Medical Missionaries of Mary (MMM) akilishwa keki.
Keki ikiliwa.
Maadhimisho hayo yakiendelea.
Mfanyakazi wa NSSF, Hakimu Mbagga kutoka Mkoa wa Kagera, akilishwa keki.
Sr Franca Ogbunuju kutoka Shirika la Srs Medical Missionaries of Mary (MMM) akimlisha keki Meneja wa NSSF Mkoa wa Singida, Oscar Kalimilwa.
Maadhimisho yakiendelea.
Meneja Rasilimali Watu na Utawala (HR)_wa Kiwanda cha Mount Meru Miller, Sara Baltazari akikabidhiwa cheti cha mwajiri bora katika kupeleka michango ya wafanyakazi wao NSSF.
Mwakilishi wa Shirika la Tree for the Future. Frank Marley akikabidhiwa cheti.
Otomali Haule kutoka Hospitali ya Makiungu, akikabidhiwa cheti.
Sr Franca Ogbunuju kutoka Shirika la Srs Medical Missionaries of Mary (MMM) akikabidhiwa cheti.
Mwakilishi wa Kanisa la Evangelist Assemblies of God Tanzania (EAGT) Kiomboi Iramba, John Leonard akikabidhiwa cheti.
Wawakilishi wa taasisi zilizofanya vizuri wakiwa na Meneja wa NSSF Mkoa wa Singida wakionesha vyeti vyao walivyotunukiwa.
Mstaafu wa NSSF Mkoa wa Singida, Joseph Gidatu akikabidhiwa zawadi.
Picha ya pamoja na mgeni rasmi wa maadhimisho hayo Meneja wa NSSF Mkoa wa Singida, Oscar Kalimilwa (katikati mbele).

No comments:

Powered by Blogger.