LIVE STREAM ADS

Header Ads

Mbunge Mattembe azindua mafunzo ya ujasiriamali Singida

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Singida, Aysharose Mattembe akizungumza na wajasiriamali wakati akizindua mafunzo ya ujasiriamali Wilaya ya Mkalama mkoani hapa Oktoba 03, 2023ambayo yatafanyika katika wilaya zote.

Na Dotto Mwaibale, Singida
Mmbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Singida, Aysharose Mattembe ameunga mkono jitihada za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan za kuhakikisha wananchi wanajikomboa kiuchumi kwa kuzindua Mafunzo ya Ujasiriamali Wilaya ya Mkalama mkoani Singida, mafunzo yenye kaulimbiu isemayo "Singida ya Ujasiriamali na Samia Inawezekana"

Akizungumza wakati akizindua mfunzo hayo Mattembe alisema yamelenga kuwawezesha wajasiriamali kujiamini na kuweza kutoka hatua moja kwenda nyingine kiuchumi.

"Mafunzo haya ambayo yatatolewa na wawezeshaji wabobezi ni muhimu sana kwa wananchi wetu na wajasiriamali kwani yanakwenda kuchochea uukuaji wa uchumi wao na kujikwamua kiuchumi" amesema Mbunge Mattembe.

Mafunzo hayo ambayo yatafanyika katika wilaya zote za Mkoa wa Singida yatahusisha usindikaji nafaka, matunda, ufugaji bora wa kuku, kilimo, pamoja na usimamizi wa fedha yameandaliwa na ofisi ya mbunge na yanatarajiwa kumalizika November 10, 2023.

Aidha Mattembe amewaomba wananchi kujitokeza kwa wingi kupata mafunzo hayo na washiriki wayazingatie kikamilifu na kuwa mabalozi wazuri kwa wengine ili tija iweze kupatikana maana ni mkombozi kwao na jamii kwa ujumla.

Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo walimshukuru Mbunge Mattembe kwa kuwajali wananchi na wajasiriamali kwa kuwapelekea mafunzo hayo yenye lengo la kuwakomboa kiuchumi na kuacha kuwa tegemezi.
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Singida, Aysharose Mattembe akionesha namna ya kupika wakati akizindua mafunzo hayo.
Mbunge Mattembe akiwa na wajasiriamali wakati wa uzinduzi wa mafunzo hayo.
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Singida, Aysharose Mattembe (wa pili kutoka kushoto waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mafunzo hayo wa Wilaya ya Mkalama.

No comments:

Powered by Blogger.